CURRENT NEWS

Thursday, July 27, 2017

RPC SHANNA -ATOA SALAMU KWA WAHALIFU WAACHE UHALIFU LASIVYO WATAKIONA


Na Mwamvua Mwinyi ,Pwani

KAMANDA wa polisi mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna ,amewapa salamu wale wenye kujihusisha na vitendo vya uhalifu mkoani hapo ,kuacha mara moja na watafute shughuli nyingine za kufanya za kuwaingizia kipato cha halali.

Amesema wameanza msako endelevu kuwasaka wahalifu mbalimbali wakiwemo majambazi ,wanyang'anyi wa kutumia silaha na Jeshi hilo halitakuwa na muhali nao pindi watakapowakamata. 

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na oparesheni hiyo iliyoanza ,kamanda Shanna alisema amejipanga na polisi wake kufanya msako uvungu kwa uvungu ili kuhakikisha wananchi waishi kwa amani na kufanya biashara na shughuli zao kwa usalama.


Aliomba ushirikiano kwa askari polisi,waandishi wa habari pamoja na jamii ili kufanikisha adhma hiyo .

Kamanda Shanna alieleza kwamba ,atakwenda ,pori kwa pori kuhakikisha wanapunguza matukio ya kiuhalifu .

Alifafanua tangu waanze msako huo july 25 mwaka huu,wameshafanikiwa kukamata mitambo mitano ya kutengeneza pombe ya moshi (gongo),pombe ya moshi lita 40 na lita 60 za Molasses , maeneo ya Lugoba, kata ya Lugoba, wilaya ya kipolisi Chalinze .

Kamanda huyo alieleza askari walimkamata Juma Ally ( 37 )na Mdunga Agustino (25 )ambaye ni dereva wa bodaboda wakiwa na mitambo hiyo na pombe .

Alibainisha watuhumiwa walikutwa na vielelezo hivyo wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki yenye namba T.399BHS aina ya SANLG.
Hata hivyo kulipatikana na vifaa vya uvuvi haramu ,eneo la Milingotini, kata ya Zinga, wilaya ya Bagamoyo .

"Kulifanyika msako maalumu wa makosa mbalimbali ukihusisha askari wa Jeshi la polisi wilaya ya Bagamoyo, PHQ,JWTZ na maafisa uvuvi na mifugo na kufanikiwa kumkamata Makamba Sixbert ( 32), mkazi wa Mlingotini "

"Mtu huyo alikutwa akiwa na scoopy  net 1, vioo vya kuogelea 3, Pipe 3, bunduki ya kuulia  samaki 1, mikuki ya kuulia samaki 3 na viatu vya kuogelea (slipers) 3, ambavyo alikuwa akivitumia kwenye uvuvi haramu." alisema .

Kamanda Shanna ,alisema kuwa walifanikiwa pia kumkamata  Doto Mwinyi ( 45 )mkazi wa Mlingotini akiwa na cylinder gas moja aliyokuwa akitumia kwa uvuvi haramu.

Wakati huo huo jeshi hilo la linamshikilia Ahmada Hassan (45) mkazi wa Gongoni na wenzake watano baada ya kuwakamata huko maeneo ya Dunda, kata ya Dunda, tarafa ya Mwambao, Bagamoyo, wakiwa na SABUFA moja aina ya KODEC inayodhaniwa kuwa ni ya wizi. 

Kamanda Shanna alisema watu hao wamefanyiwa mahojiano na wamekiri kujihusisha na matukio ya uvunjaji na uporaji nyakati za usiku kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Mwisho
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania