CURRENT NEWS

Tuesday, July 4, 2017

WAJASIRIAMALI WAIONA NEEMA KUPITIA MAVUNDE

Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akikaribishwa na  Mkurugenzi mkuu wa Mjasiriamali Kwanza Dk.Mujungu katika ufunguzi wa Kongamano.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akiangalia CD mafunzo ya ujasiriamali

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wajasiriamali kwenye Kongamano Elimu ya ujasiriamali. 

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wajasiriamali 

 Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wajasiriamali 
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wajasiriamali 

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wajasiriamali 
.......................................................................
Mbunge wa Dodoma mjini,Anthony Mavunde ameahidi kuvitafutia fursa ya mikopo na mitaji vikundi vya ujasiriamali ili kufanya shughuli zao mbalimbali za ujasiriamali.

Mavunde ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mjasiriamali Kwanza.

Kongamano hilo limejumuisha zaidi ya wananchi takribani 2000 ambao wanapatiwa mafunzo ya kutengeneza bidhaa na kupata elimu ya ujasiriamali kwa siku nne na baadaye kuunda na kusajili vikundi vyao vya ujasiriamali.

Amefafanua kwa kuanzia wataanza kwa kugawa kwa vikundi mbalimbali mashine za kutengeneza chaki,mashine ya kutotolesha mayai(Incubators),mashine ya kutengeneza tofali,mashine za kunyonyoa manyoya ya kuku(chicken pluckers),mashine ya kushonea,mashine ya kukamua juice ya miwa,mashine ya kutengeneza popcorn na mashine ya kuchapisha(heat press) vyote vyenye jumla ya shilingi 52,000,000.

Kupitia mpango huo,amesema wakazi wa jimbo la Dodoma Mjini watapata fursa ya kukuza uchumi wao wa mtu mmoja mmoja na hivyo kujiongezea kipato na kuchangamkia fursa ya uwepo wa makao makuu ya Serikali Dodoma.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania