CURRENT NEWS

Wednesday, August 2, 2017

DAWASCO YASHAURIWA KUTOA HUDUMA KWA UWAZI

Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.  PICHA NA KAJUNASON BLOG/MMG.
Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco).
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa na watendaji wengine wakati wakiimba wimbo wa 'Tanzani', 'Tanzania'.
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema ameapa kuwashughulikia watumishi wachache chini ya wizara yake ambao bado wanaendekeza maisha ya ujanja ujanja kazini. 

 Profesa Kitila ameitoa kauli hiyo leo Jumanne wakati akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) kwenye ofisi za makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. 

 Amesema ingawa Dawasco imefanikiwa kuboresha huduma zake, lakini wapo watumishi wa chache ambao bado wanafanya kazi kwa ubabaishaji. 

 Amesisitiza kuwa zama za ujanjaujanja zimekwisha na wale wachache wanaoshiriki mbinu za kulihujumu shirika hilo hawatavumiliwa na watendaji wa shirika hilo kutoa taarifa kwa watakaobainika. 

 Wakati huo mhuo, Profesa Mkumbo amewashukuru watendaji na watumishi wa Dawasco akibainisha kuwa siku hizi simu za malalamiko anazopigiwa na wateja kuhusu huduma za maji zinazotolewa na Shirika hilo zimepungua sana. Amesema hali hiyo inatokana na Dawasco kuboresha huduma zake. 

 Amesema hivi sasa anatumiwa ujumbe mfupi wa kupongezwa kuhusu huduma za zinatolewa na Dawasco na kulitaka shirika hilo kuendelea kuchapa kazi ya kutoa ya kuwahudumia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. “Hongereni kwa huduma nzuri mnazitoa kwa wakazi wa mikoa hii. 

Nyie ndiyo taswira ya Serikali katika utoaji wa huduma za maji. Bila nyie Ukatibu wa Mkuu hauna maana kwa mkoa wa Dar es Salaam hata waziri na wizara kwa ujumla,” amesema Profesa Mkumbo.

 Profesa Mkumbo amesema wizara yake haina mipaka katika utendaji kazi na kwamba ipo wazi kuwasiliana mtendaji yeyote atakayetaka huduma.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania