CURRENT NEWS

Monday, August 21, 2017

SHAKA AMALIZA ZIRA YA KIKZAZI PEMBA, AMTUMIA SALAMU MAALIM SEIFKaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.


Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.


Na Mathias Canal, Pemba

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amehitimisha ziara ya siku nne ya kikazi Kisiwani Pemba-Zanzibar  kwa kuzuru katika Mikoa yote miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba na Wilaya zake zote za Wete, Mkoani, Chakechake na Micheweni.

Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengi alikagua na kushiriki kufanya kazi za kijamii ikiwa  ni  pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020, kushiriki kuona shughuli mbali mbali za uzalishaji Mali kupitia makundi ya vijana na kuwasaidia kwa kuwaunga mkono ili kuongeza  mtaji  wa miradi yao.

Alitumia ziara hiyo kuzungumza na makundi ya vijana kwa nyakati tofauti,  viongozi wa CCM, jumuiya za CCM Pamoja na kushiriki shughuli zingine mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa na kuwaasa kukaa maskani pekee pasina kufanya kazi za uzalishaji mali jambo ambalo litapeleka mbele maendeleo katika jamii.

Katika maeneo yote aliyozuru Kaimu Katibu Mkuu huyo alitilia zaidi msisitizo kwa vijana kujiunga na vikundi mbalimbali vya kijamii ili kupatiwa mikopo ya vijana inayotolewa na serikali kwa asilimia 5 kila mwezi.

SALAMU KWA MALIM SEIF 

Katika hatua nyingine Shaka alimtumia salaamu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF aliyesimamishwa uongozi Maalim Seif Shariff  Hamad kwa kumtaka kuacha kueneza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao kwani kuhubiri siasa za mgawanyiko ni utaratibu wa kiongozi asiyekuwa mweledi kwani maendeleo hayahitaji ubaguzi dhidi ya wananchi.

"Juhudi za SMZ na SMT katika kuwatumikia wananchi hazitadumazwa kwa maneno ya wapinzani badala yake zitaendeleza mikakati yake ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka" Alisema Shaka

Alisema ni Siasa uchwara kuhubiri mgawanyiko katika jamii na kutumia nasaba na asili ili kusaka madaraka, kiongozi ambaye atajiegemeza katika siasa chafu milele hawezi kupata ridhaa ya wananchi.

"Nimeshiriki ujenzi wa shina hili nikiwa na furaha kwenye mtima wangu, Msisahau kumpelekea salamu Maalim Seif Shariff Hamad mwambieni asichoke kueneza siasa za mgawanyiko CCM na serikali zake haizitaacha kabisa kuwapelekea maendeleo wananchi bila kuwabagua" Alisema Shaka 

Shaka alisema kuwa Kiongozi au mwanasiasa anayekusudia kupata imani na amana ya wananchi hawezi kushiriki kuwagawa watu bali huwa kiranja wa kuwaunganisha na kuwataka wawe wamoja huku wakiishi kwa maelewano na mshikamano.

Alisema kuwa Wakati dunia, vyama vya siasa makini, wanaharakati na mashirika ya kimataifa yakihubiri uwepo wa amani, maelewano na kukataa mgawanyiko, itashangaza kumsikia mtu anayejiita kiongozi akihubiri siasa chafu za mgaanyiko na mifarakano.

"Tunamsubiri tena Seif Sharif Hamad mwaka 2020 tumpige mara ya saba, sijui atawania Urais kwa CUF ipi, ile ya Profesa Lipumba haimtaki, yake yeye haitambuliwi na Msajili wala hana Bodi ya Wadhamini, akija tutamgaragaza ili aje kupumzika Mtambwe " Alisema Shaka

Ziara ya  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka imeacha gumzo kubwa kwa wananchi kufunguka kiakili na kumualika tena kwa mara nyingine kwani tayari wamewelewa namna wanavyopotoshwa na viongozi wa vyama vya upinzani.

MWISHO.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania