CURRENT NEWS

Wednesday, August 2, 2017

SIMBACHAWENE: SEKTA YA KILIMO BADO NI MUHIMILI WA UCHUMI TANZANIA

Na Mathias Canal, Lindi

Sekta ya Kilimo imetajwa kuwa bado ni muhimili wa uchumi wa Tanzania kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia  65.5  ya Watanzania na kuchangia zaidi ya asilimia 100 ya chakula hapa nchi katika miaka yenye mvua ya kutosha. 

Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, kwa mwaka huu wa 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, tarehe 1/8/2017.

Alisema Kaulimbiu ya Nane Nane mwaka huu inasema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati”. Kaulimbiu hii inahamasisha Wakulima, Wafugaji na Wafugaji kuongeza uzalishaji na tija katika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Mhe Simbachawene alisema kuwa mwaka 2015, Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29 ya pato la Taifa, na mwaka 2016 ilichangia asilimia 29.1. Hivyo, ni dhahiri kuwa mchango mkubwa katika pato la Taifa ulitokana na Sekta ya Kilimo ukifuatiwa na Sekta nyingine za kiuchumi. 

Alisema Kutokana na umuhimu huo, Serikali inaeendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza kasi ya kukuza kilimo, mifugo na uvuvi ili kuchochea na kufikia uchumi wa viwanda sawasawa na Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano. 

Alisema kuwa Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2016 uliongezeka kufikia kiwango cha utoshelevu wa asilimia 123 ikiwa ni zaidi ya kiwango cha asilimia 120 cha mwaka 2015.  

Hali hiyo, imechangiwa na ongezeko la asilimia 6.7 la uzalishaji wa mazao ya nafaka yakiwemo mahindi na mchele. Usalama wa chakula pia unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mazao yasiyo nafaka kama vile mihogo, viazi, ndizi na mazao ya jamii ya mikunde ambayo kwa ujumla kulikuwa na ongezeko la uzalishaji wa asilimia 1.5

Pamoja na kiwango cha kuridhisha cha uzalishaji wa mazao ya chakula, Mhe Simbachawene alisema kuwa hali mbaya ya hewa iliyojitokeza mwisho wa mwaka 2016 na mwanzoni mwa mwaka 2017 ilisababisha kupanda kwa bei za chakula katika maeneo mbalimbali ya nchi. 

Hata hivyo Katika kukabiliana na hali ya ukame uliotokana na uhaba wa mvua za vuli na kuchelewa kuanza kwa mvua za masika katika baadhi ya maeneo, hatua sitahiki zilichukuliwa. 

Amezitaja Baadhi ya hatua hizo kuwa  ni pamoja na kusambaza mbegu bora zinazokomaa kwa muda mfupi, zikiwemo mahindi, mtama na mpunga huku vipando vikiwemo pingili za mihogo na viazi vitamu vilisambazwa.

"Nchi yetu imebahatika kuwa na idadi kubwa ya mifugo ikiwemo ngómbe, kondoo, mbuzi, kuku wa asili na kuku wa kisasa. Pamoja na kuwa na idadi kubwa ya mifugo, viwango vya ulaji wa mazao ya mifugo hususani nyama, maziwa na mayai bado viko chini. Katika mwaka 2016, mifugo inayouzwa katika minada iliongezeka ukilinganisha na mwaka 2015 na hivyo kupata mapato yanayotokana na ng’ombe shilingi trilioni 1.34, mbuzi na kondoo shilingi trilioni 1.02" Alisema Mhe Simbachawene

Aliongeza kuwa Mapato yanayotokana na mauzo ya ngozi yalifikia shilingi bilioni 34.7 kwa ngozi ya ngómbe, shilingi bilioni 6.2 kwa ngozi ya mbuzi na kondoo. Mapato yanayotokana na uzalishaji wa malisho katika mashamba ya Serikali yalifikia shilingi bilioni 1.14. Aidha, mapato yanayotokana na uzalishaji wa mbegu za malisho bora ya nyasi  yalifikia shilingi milioni 55.8 na jamii ya mikunde shilini milioni 11.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) akizungumza na Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.(Picha Zote na Mathias Canal) 
Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB), Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb), na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Halima Dendego wakitazama namna ya uzalishaji samaki katika banda la JKT wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) akizungumza na Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Halima Dendego akitoa salamu za mkoa wa Lindi na Mtwara wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) akisisitiza jambo alipozuru katika ukumbi wa JKT wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (Mb) akionyesha moja ya mazao yanayozalishwa katika banda la JKT wakati wa  maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew Mtigumwe akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (Mb) akizungumza na Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango (Kushoto) akijadili jambo na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Lindi, Mhe Fatuma Mikidadi mara baada ya hotuba ya  Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (Mb) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017. 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania