CURRENT NEWS

Saturday, August 19, 2017

UVCCM YALAANI UBAGUZI MISIKITINI PEMBA

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumzia kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza taarifa ya kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
Wanachama wakimlaki Kaimu katibu mkuu mara baada ya kuwasili  kuzungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM umelaani vikali ubaguzi uliofanywa na baadhi ya Wanachama wasikuwa CCM kwa kuwazuia wanachama wa CCM kuswali pomoja katika misikiti kwenye baadhi ya maeneo Mbalimbali visiwani Pemba.

Umoja huo umesema kuwa kuzuia watu kuswali kisa itikadi za dini zao ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani kufanya hivyo ni kupiga amri ya Mwenyezi Mungu anayetoa onyo Kali katika Quran kwa wale wanaothubutu kuwazuia waini wengine kuswali.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka Wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Wakati alipotembelea Msikiti wa Masjid Lmuhajiriina uliopo Eneo la Kiungoni Kimango Wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema kuwa Imani ya dini yoyote nchini haibagui wala kuchagua watu kuswali kutokana na Itikadi zao za kisiasa ama kikabila kwani dini Ni ibada ya Imani kwa kila mwananchi.

Shaka Alisema kuzuia watu kuabudu Ni makosa kwa mujibu wa taratibu za nchi lakini pia ni Dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani hakuna maandiko yanazuia watu kushiriki katika ibada.

Mnamo Mwaka Mwaka 2016 baada ya kura ya marejeo kikundo Cha watu wachache katika baadhi ya maeneo walianza kuwashawishi Wananchi kususia kuswali na Wanachama wanaotokana na CCM ambapo kwa kiasi kikubwa waliwaunga mkono Jambo lililopelekea waumini was kiislamu watokanao na CCM kuanza kusali majumbani mwao.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania