CURRENT NEWS

Friday, August 4, 2017

VIONGOZI WILAYA YA MALINYI WATAKIWA KUJISAHIHISHA


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi katika Halmashauri ya wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua nyumba za walimu katika wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Malinyi Haji Mponda na baadhi ya viongozi wa serikali wakikagua Mradi wa maji.

Wanafunzi wa shule ya sekondari wilayani Malinyi wakimsikiliza Nabu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea katika wilaya hiyo.

...............................................................................................
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewataka viongozi na watendaji ndani halmashauri ya wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro kujitathmini kufuatia kuwepo na mahusiano mabaya kati ya mkurugenzi na wakuu wake wa Idara na baina ya mkurugenzi na mkuu wa wilaya.


 Jafo aliyasema hayo leo hii alipokuwa katika ziara ya kikazi wilayani humo na katika kikao chake na watumishi wa wilaya hiyo.


Katika kikao hicho, Naibu Waziri Jafo alipokea malalamiko kuwa mkurugenzi wa halmashauri huyo Maselin Ndimwa anatuhumiwa kwa kuendesha halmashauri kinyume cha utaratibu kwa kunyanyasa watumishi na kushindwa kuitisha vikao vya kisheria kwa mujibu wa sheria.


Aidha Jafo alisema kuna malalamiko mkurugenzi asikilizi lolote kutoka kwa Mkuu wa wilaya na kumekuwa na hali mbaya sana ya mahusiano Wilayani humo hali inayosababisha maendeleo kuchelewa.


Kufuatia hali hiyo, Jafo amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kujitathmini na kufanya marekebisho ya kiutendaji katika Ofisi yake.


 Pia Naibu Waziri huyo ametoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya hiyo Majura kasika kusimamia mwenendo mzima wa wilaya hiyo na kuijulisha Ofisi ya Rais Tamisemi mwenendo wa kimahusiano katika halmashauri ya Malinyi.  


Amewataka watumishi wa halmashauri ya Malinyi kufanyakazi kwa kujituma ili kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania