CURRENT NEWS

Thursday, August 24, 2017

WANANCHI WA DOLOLO WAISHUKURU SERIKALI YA MAGUFULI

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Kologombe ambalo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja ya Nyatanga lililopo katika kijiji cha Nyani wilayani Kisarawe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo ya ujenzi wa barabara ya Mzenga-Gwata.
Ujenzi unaoendelea wa daraja la Kologombe wilayani Kisarawe

...........................................................................
WANANCHI wa vijiji vya Dololo na Gwata katika kata ya Mafizi wilayani Kisarawe wameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli wa kuwaboresha barabara inayotoka Mzenga hadi Dololo kupitia Gwata. 

Wakazi hao walitoa shukurani hizo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofanywa na Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo.

Wamemshukuru Mbunge wao kwa kuwapigania ambapo kwasasa barabara hiyo inaboreshwa kwa kuweka  vizuri katika maeneo korofi na kukamilisha ujenzi wa madaraja mawili la kipora, Nyatanga, na kwasasa serikali inakamilisha ujenzi wa daraja la Kologombe.

Akizungumza na wananchi hao, Naibu Waziri Jafo amewapongeza viongozi na watendaji kwa kusimamia vyema miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani humo.


Aidha amewapongeza  wakandarasi wanaojenga daraja la Kologombe kwa kazi nzuri ya ujenzi wa daraja hilo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania