CURRENT NEWS

Monday, September 18, 2017

DK. SHEIN KUONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM, KESHO MJINI ZANZIBAR


Dk. Shein
ZANZIBAR
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, inatarajiwa kufanya kikao chake kesho Septemba 18 mwaka huu, chini ya Makamu  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar  Dk. Ali Mohamed Shein.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Waride Bakari Jabu,  imesema kikao hicho cha siku moja kitafanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi. 

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitapokea na kujadili kwa kina taarifa ya Hali ya Kisiasa ya Zanzibar pamoja na taarifa nyengine mbali mbali kutoka Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, vile vile kikao hicho kitapokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika ngazi za Wilaya kwa kipindi cha 2017-2022, kwa upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa. 

Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC - Zanzibar kilichofanyika Septemba 16, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”, kwa ajili ya kuandaa Ajenda za kikao hicho.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania