CURRENT NEWS

Tuesday, September 19, 2017

JAFO AWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI DODOMA.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiongea na viongozi wa dini mjini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiongea na viongozi wa dini mjini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiongea na viongozi wa dini mjini Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini.

Wanasemina wakifuatilia maelekezo katika semina ya siku tatu ya viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Dodoma
.......................................................................
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa dini kwakuwa mstari wa mbele katika kuliombea Taifa na kuwaomba kuendelea na moyo huo na kukemea vitendo viovu.

Jafo ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika semina ya siku tatu ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kikiristo mkoani Dodoma.

Naibu Waziri Jafo amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kusimamia maadili kwa kuendelea kukemea matendo maovu yakiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, rushwa na mauaji ya vikongwe.

Aidha Jafo amewaomba viongozi hao wa dini kupinga mambo yote yasiyo mpendeza mungu.

Akizuzungumzia kuhusu amani na utulivu hapa nchini, Jafo amesema kwasasa nchi inapoelekea katika uchumi wa viwanda ni vyema viongozi hao wakaendelea kuliombea Taifa kwa kuwa bila amani malengo hayawezi kufikiwa.


“Nawaomba pia muendelee kumuombea Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayo ifanya kwa manufaa ya wananchi wote,”amesema Jafo

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania