CURRENT NEWS

Friday, September 29, 2017

JAFO: TUWALINDE WAZEE WETU DHIDI YA MAUAJI

Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizindua rasmi Maadhimisho ya siku ya wazee yaliyozinduliwa kitaifa katika viwanja cha Nyerere Square Mkoani Dodoma.


Mmoja wa wazee Mzee Kachenje akitoa neno la shukrani katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani.


Baadhi ya wazee waliohudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani.


Baadhi ya wazee waliohudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani.


Baadhi ya wazee waliohudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani.
 .......................................................................................
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ametoa maagizo kwa ngapi za mikoa na wilaya kusimama imara katika kuwalinde wazee dhidi ya mauaji ya kikatili yanayofanywa na watu wasio na roho za ubinadamu. 

Jafo aliyasema hayo leo alipokuwa akizindua rasmi Maadhimisho ya siku ya wazee yaliyozinduliwa kitaifa katika viwanja cha Nyerere Square Mkoani Dodoma. 

Amesema serikali inasikitishwa na Mauaji wa wazee ambayo yamekuwa yakiendelea hususan katika mikoa ya kanda ya ziwa kitendo kinacho ashiria unyama uliopitiliza.

Jafo amekemea tabia hiyo mbaya ambayo inaharibu sifa ya nchi na utamaduni.

Kutokana na hali hiyo, Jafo amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kupitia kamati zao za ulinzi na usalama kuwachukulia hatua kali watu wote wanaoendesha vitendo hivyo viovu hapa nchini. 


Maadhimisho hayo yamezinduliwa rasmi Leo kitaifa ambapo wazee mbalimbali wamepata fursa ya kupimwa afya zao bure katika viwanja hivyo na kilele chake cha kitafanyika Oktoba mosi, mwaka huu.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania