CURRENT NEWS

Friday, September 1, 2017

KAMATI ZA BUNGE ZA HESABU ZA SERIKALI, NISHATI NA MADINI NA MIUNDOMBINU ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jaffo (aliesimama)akizungumza jambo pale Watendaji wakuu kutoka ofisi hiyo walipokutana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali leo Mjini Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Ndg. Kapulya Musomba akizungumza jambo pale kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipokutana na Watendaji wakuu kutoka Shirika hilo, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na REA leo Mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia majadiliano baina yao na Watendaji wakuu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wizara ya Nishati na Madini pamoja na REA leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (aliesimama) akizungumza na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Watendaji wakuu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wizara ya Nishati na Madini pamoja na REA (hawapo kwenye picha) leo Mjini Dodoma. katikati ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Deo Ngalawa na kulia ni Katibu kamati wa kamati hiyo, Ndg. Felista Mgonja
 Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Deo Ngalawa (katikati)akizungumza jambo pale kamati hiyo ilipokutana na Watendaji wakuu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na REA wakijadili taarifa kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi na Usambazaji wa Gesi Asilia nchini pamoja na Utekelezaji wa Miradi ya REA Awamu ya Tatu pamoja na Utatuzi wa Changamoto za Ukamilishaji wa Miradi wa Awamu ya I na II. Kushoto, ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani na kulia ni Katibu kamati wa kamati hiyo, Ndg. Felista Mgonja
 Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Ndg. Salome Makamba akizungumza jambo pale kamati hiyo ikifanya uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa sita, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma. kulia Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Daniel Mtuka
 Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Tundu Lissu akisisitiza jambo pale kamati hiyo ikifanya uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa sita, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma, kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Salome Makamba
 Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Leonidas Gama akizungumza na Wajumbe wa kamati wakati kamati hiyo ikifanya uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa sita, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma, kulia ni katibu kamati wa kamati hiyo, Ndg. Yona kirumbi
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Prof. Norman Sigara king akisisitiza jambo pale kamati hiyo ilipofanya majadiliano baina yao na Watendaji Wakuu kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, TCRA, Vodacom, Airtel na Tigo (hawapo kwenye picha) katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma. kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Edwin Ngonyani.
 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakifuatilia Majadiliano baina yao na Watendaji Wakuu kutoka TCRA, Vodacom, Airtel na Tigo katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania