CURRENT NEWS

Friday, September 1, 2017

MAHAKAMA YA JUU NCHINI KENYA YAFUTA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS

  1. Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo akiwa na kura 8,203,290 (54.27%)

  1. Tume ya uchaguzi ilisema Raila Odinga alipata kura 6,762,224 (44.74%)

Mgombea urais wa upinzani Raila Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika.
Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais.
Imetoa mfano mwema.
"Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan."
Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania