CURRENT NEWS

Tuesday, September 5, 2017

MSAJILI WA HAZINA AYATAKA MASHIRIKA YA UMMA KUJIENDESHA KIMKAKATI

 Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu wa taasisi hizo (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini mkataba wa utendaji kazi kwa taasisi hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili kulia) wakiweka saini katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.
 Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili kulia) mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.
 Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) wakiweka saini katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 
Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu wa taasisi hizo wakimsikiliza Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini mikataba ya utendaji kazi kwa taasisi na Mashirika ya Umma mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Na.Bushiri Matenda-MAELEZO
Ofisi ya Msajili wa Hazina inasema kuwa Taasisi na Mashirika ya Umma sasa rasmi kutekeleza mkakati wa utendaji kazi ili kujiendesha na kutoa gawio kwa Serikali yenye lengo la kuchochea maendeleo kwa taifa na kuendelea kuboresha huduma bora za kijamii.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Msajili Mkuu wa Hazina Dkt.Oswad Mashindano wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa utendaji kazi baina  ya Msajili wa Hazina na baadhi ya Wenyeviti wa bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini. 
“Ofisi ya Hazina inasimamia Taasisi mbalimbali takribani 265, ni vyema Taasisi hizo kwa kushirikiana kwa pamoja zikasimamiwa vizuri ili kutoa huduma endelevu na kuchangia katika uwekezaji wenye tija kwa taifa”,alisema Dkt.Mashindano.
Aidha alisema kuwa mwaka 2014-2015 Ofisi ya msajili wa hazina walifunga mkataba naTaasisi na Mashirika ya Umma 71 kati ya 265 ambapo mkataba huo ulilenga katika maeneo  manne ya kiutendaji ambayo ni usimamizi katika rasilimali fedha , watu, utawala bora na huduma kwa wateja.
Dkt. Mashindano aliongeza kuwa Katika tathmini ya mkataba uliopita kupitia nyaraka  mbalimbali , uchambuzi umeonyesha kuwa  zipo baadhi ya dosari katika utekelezaji wa makubaliano  ya awali  ambazo alizitaja kuwa asilimia 25 ya mpango mkakati  waliojiwekea Taasisi na Mashirika hayaendani na  bajeti  waliojiwekea.
Pili malengo yaliyobainishwa na Taasisis hizo  hayaendani na mpango kazi , maeneo ya ya usimamizi wa rasilimali watu na utawala bado kuna changamoto, eneo la ukusanyaji mapato katika baadhi ya Taasisi bado ni ndogo pamoja na  eneo la Huduma kwa wateja linahitaji kusimamiwa ipasavyo na kuwepo kwa baadhi ya Taasisi na Mashirika ya Umma kujaza matokeo ya kazi ambazo hazipo kwenye utekelezaji wa mapango kazi.
“Katika utiaji wa  sahihi, mkataba huu unaohusisha zaidi ya Taasisi na Mashirika 30  naamini tutazingatia kutatua changamoto zilizopo na kuweka mpango wa maendeleo endelevu”, alisisitiza Dkt. Mashindano.
Naye spika wa bunge mstaafu ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa bima wa afya Bi. Anna Makinda  alitoa neno kwa niaba ya wenyeviti wa Bodi wa Taasisi na Mashirika ya Umma alisema  ni vizuri tukatatua changamoto zilizojitokeza katika uendeshaji wa mashirika ya Umma ili yajiendeshe kwa tija na maslahi ya Taifa.
“Watendaji wakuu wa Taasisi za Umma na wenyeviti wa Bodi tunawajibishwa na makubaliano haya, tunategemewa sana katika kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa ujumla”, alisema Bi. Makinda. 
Aliongeza kuwa Taasisi za vyuo vikuu vilivyoingia makubaliano haya watawajibika katika kuwatayarisha vijana katika kuliletea Taifa maendeleo.  
Wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo iliyopo taratibu na Sheria zilizopo kwa kushirikiana na Ofisi ya Hazina ili kuleta tija kwa watumishi wengine katika Taasisi za Umma. 
Mbali na majukumu iliyonayo Ofisi ya Msajili wa Hazina pia inasimamia katika masuala yote ya uwekezaji nchini, mitaji, malipo mbalimbali ikiwemo mishahara kwa watumishi wa Umma.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania