CURRENT NEWS

Thursday, September 7, 2017

MTOTO WA KIKE WA MIAKA MITANO AKATWA NA KISU KICHWANI NA BABA YAKE WA KUFIKIA -RPC SHANNA


Abdallah  Machupa, (49 )fundi ujenzi, mkazi wa Kongowe ,anaedaiwa kumkata kisu mara mbili mtoto wake wa kufikia wa kike mwenye miaka mitano kwa kosa la kuiba mayai mawili .(picha na Mwamvua Mwinyi)

MTOTO wa kike (5)mwanafunzi wa shule ya awali Kongowe Kibaha mkoani Pwani ,amejeruhiwa kwa kukatwa kisu mara mbili kichwani na baba yake wa kambo Abdallah Machupa (49)kwa kosa la kuiba mayai mawili .

Kufuatia kitendo hicho cha kikatili kwa mtoto ,baba huyo anashikiliwa na polisi huku akitarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili .

Akizungumzia kuhusu tukio hilo ,kamanda wa polisi mkoani hapa ,(ACP)Jonathan Shanna ,alikemea tabia za kunyanyasa watoto na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.

Alifafanua kwamba ,september 4 majira ya saa mbili usiku mtoto huyo,alituhumiwa kuiba mayai mawili kwa bibi Baby.

"Taarifa zilifika kwa mama mzazi aitwaye Hadija  ambaye alimkanya mwanae kwa kumchapa viboko na kumwacha"

"Kufika tarehe 5 september mwaka huu saa 9 jioni baba wa kufikia wa mtoto huyo Abdallah  Machupa ambae ni fundi ujenzi, mkazi wa Kongowe; alipata taarifa hizo mtaani akarudi nyumbani na kuanza kumchapa kwa fimbo" alisema kamanda Shanna.

Kamanda Shanna alisema , kama haitoshi baba huyo wa kufikia akachukua panga lakini kaka yake na aliyejeruhiwa mwenye umri wa miaka 8 Hamis Abdallah akamzuia baba yao ,ndipo baba akachua kisu na kumkata kichwani mara mbili.

Alisema wananchi waliingilia kati kumwokoa mtoto huyo,,hata hivyo walimshambulia kwa kumjeruhi Abdallah kichwani na  kisogoni.

Kamanda Shanna ,alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa yupo mahabusu na wote wawili walitibiwa hospitali ya  rufaa ya mkoa ya Tumbi.

Kwa upande wa wananchi waliokuwepo eneo la Tukio akiwemo Carolina Kisada ,alisema wazazi waache hasira kwa watoto ambao wanaweza kuadhibiwa kwa adhabu nyepesi kama kuchapwa viboko kuliko kutumia nguvu .

Alisema baba huyo achukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wazazi wasio na huruma.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania