CURRENT NEWS

Friday, September 1, 2017

SERIKALI MKOANI PWANI YAZIASA TAASISI ZINAZOWEKA URASIMU KWA WAWEKEZAJI

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI mkoani Pwani,imeziasa baadhi ya taasisi na idara zinazoweka mazingira ya urasimu wakati wa kutoa vibali vya ujenzi  na hati  miliki kwa wawekezaji.

Aidha wananchi mkoani hapo wametakiwa kujiongeza katika elimu mbalimbali,ujuzi na kuwa wavumilivu kazini kwani ni asilimia 20 pekee wanaoonekana kumudu kufanya kazi viwandani na asilimia 80 ni kutoka nje.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo , akizungumza na wawekezaji na viongozi mbalimbali wa serikali na wawakilishi kutoka taasisi zinazoshughulikia masuala ya uwekezaji na ujenzi wa viwanda,alisema urasimu unakwamisha juhudi za uwekezaji.
Alisema ni lazima mwekezaji apatiwe kibali baada ya kupata ardhi na pia kuwepo kwa utaratibu mzuri wa kuwapa vibali vya kazi .
Alieleza wakati wakivutiwa wawekezaji na viwanda viendeshwe ili kukuza sekta hiyo na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.
Hata hivyo,mhandisi Ndikilo alifafanua NEMC na EIA ni ishu/tatizo ,malalamiko mengi anapokea kutoka kwa wawekezaji kuhusiana na eneo hilo hivyo nazo zinakila sababu ya kujirekebisha pale wanapotolewa dosari ili kuondoa kero zinazowagusa.
“Nipongeze mchango wa serikali za mitaa  kwa mchango wao mkubwa wa kukuza sekta ya uwekezaji na kuondoa urasimu”.
“Kwanini kuna urasimu kwenye kupata vibali kwa wawekezaji,wengi wanalalamika na kuniletea kero hiyo ,naomba ifanyiwe kazi,ili isiwe kazi kupata vibali hivyo”.
“Sheria za kazi sanjali na mazingira zipo,waelimisheni hawa wajue wanayotakiwa kuyafuata pasipo kuwabana,wanacomplain kuwa wanapata ardhi:,wana TIN namba ,lakini NEMC/EIA ni ishu,mgogoro mkubwa,why,toeni utaratibu unaotumika na washughulikieni kwa wakati’alisema mhandisi Ndikilo.
Akizungumzia lengo la kuitisha mkutano huo,alisema ni kujua changamoto zinazowakabili wawekezaji ili serikali ,idara ,taasisi na vitengo husika vinavyoshughulikia masuala ya uwekezaji ama ujenzi wa viwanda utatue changamoto hizo.

Mkuu huyo wa mkoa,alielezea, mkutano huo umefungua ukurasa mpya hivyo itakuwa vizuri kuitisha mkutano wa aina hiyo mara kwa mara  pasipo kusubiri mkutano rasmi.
Alisema uwekezaji umefungua fursa za ajira kwa vijana na wananchi wengine kijumla,kuinua pato la mkoa na taifa ,kuinua uchumi.
Nae katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji,Shangwe Twamala ,alisema kuna kila sababu ya kufanyika kwa maboresho kwa taasisi zinazoguswa kuwa na vipingamizi ili kukuza sekta ya viwanda.
Mbali na hilo, alisema zipo fursa ya uwekezaji  lakini wazazi na vijana bado hawajatambua kujipanga kukuza elimu na ujuzi wao kwa ajili ya kujipatia ajira kirahisi.
Akizungumzia suala la miundombinu na maji ,Twamala alisema ni changamoto nyingine zinazowakwamisha wawekezaji .
Juni 21 mwaka huu ,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,Dk.John Magufuli,akiwa katika ziara ya kutembelea na kuzindua viwanda mkoani Pwani,alikemea baadhi ya taasisi zinazoweka mazingira ya rushwa na urasimu wakati wa kutoa vibali kwa wawekezaji ikiwemo OSHA,NEMC na shirika la viwango TBS.
Alisema,suala la vibali ameliona na anataka asikie kuna mwekezaji amebaniwa kibali ,ili atakaebainika amshughulikie . 
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania