CURRENT NEWS

Sunday, September 10, 2017

VIONGOZI WILAYA YA MPWAPWA WAISHUKURU SERIKALI


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua majengo yaliyo karabatiwa na serikali katika sekondari ya mpwapwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua jiko la kisasa linalo jengwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wa Mpwapwa sekondari.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Kamati ya ujenzi wa Mpwapwa sekondari.

Baadhi ya madarasa ya Mpwapwa sekondari yaliyo karabatiwa.
 .................................................................................
VIONGOZI wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameishukuru serikali kwa kukarabati sekondari ya Mpwapwa ambayo majengo yake yalikuwa yana hali mbaya.

Viongozi hao wametoa shukrani hiyo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua ukarabati wa shule hiyo.

Shule hiyo ni miongoni mwa shule 88 kongwe zinazokarabatiwa na serikali ambapo katika awamu ya kwanza ukarabati umeanza kwa shule 43.

Katika shule hiyo, Serikali imefanikiwa kujenga bweni moja jipya la wasichana, ukarabati wa mabweni 12 ya wavulana, ukarabati wa vyumba vya madarasa 22, bwalo la chakuka pamoja na jiko, maktaba, maabara tatu, ofisi za walimu, mfumo wa maji na umeme ambapo jumla ya sh.bilioni 1.2 zimetumika.

Akizungumza na viongozi katika ziara yake,Naibu Waziri Jafo ameipongeza Kamati ya ujenzi kwa kufanyakazi bila kuchoka na kufanikisha kuibadili kabisa shule hiyo ambayo kwasasa imegeuka kuwa shule bora ya kisasa tofauti na ilivyokuwa awali.

Naibu Waziri Jafo amewataka wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii kwani serikali ya Dk. John Magufuli imeamua kuboresha miundombinu pamoja na vifaa vya kutolea elimu kwa lengo la kufanikisha elimu bora hapa nchini.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania