CURRENT NEWS

Saturday, September 23, 2017

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE KILIMO , MIFUGO ,UVUVI NA MAJI WAVUTIWA NA HUDUMA NZURI ZA IRINGA SUNSET HOTELI

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  akipokelewa na mkurugenzi wa    Iringa Sunset Hotel  Batsta Filipatali wakati wa  chakula cha jioni  kilichoandaliwa na ofisi ya  mkuu  wa  mkoa kwa  wajumbe wa  Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji,
Maandalizi ya  chakula  katika   Iringa Sunset  Hoteli  kwa  ajili ya  wajumbe  wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji,
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  akifurahia  maandalizi ya  wageni  wake katika   ukumbi wa   Iringa Sunset Hoteli
Mkurugenzi wa Iringa Sun Set  Hoteli  Bw  Filipatali katikati  akiwa na  wafanyakazi wake  wakati wa maandalizi  ya  chakula cha Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji,
Mkurugenzi  wa Iringa  Sunset  Hoteli  akiwakaribisha  mkuu  wa  mkoa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji,
Wahudumu  wakifurahia  kwa maandalizi
Tumebobea kwa  huduma  bora ya
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji,wakipata chakula  kilichoandaliwa na ofisi ya  RC  Iringa ukumbi wa Iringa Sunset Hoteli  Gangilonga  Iringa mjini
Mmoja kati ya  wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji,akipongeza  kwa  huduma nzuri
Wajumbe  wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji,pamoja na  wadau wa Kilimo mkoa  wa Iringa wakiwa katika mazungumzo
Uongozi  wa  Iringa  SunSet Hoteli  umepongeza jitihada za serikali ya  mkoa  wa Iringa kuendelea  kukuza  sekta  ya  utalii katika  mkoa  huo  kwa  kuwafikisha  wageni  mbali mbali  wakiwemo  wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji katika  hoteli  hiyo  ambayo ni  moja kati ya  Hoteli  za  kitalii mkoani Iringa.

Mkurugenzi  mtemndaji wa  Iringa  SunsetHotel Batsta Filipatali  aliyasema  hayo  baada  ya pongezi kutoka kwa wajumbe  wa kamati  ya 
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji kufika  kupata   huduma ya  chakula  cha  jioni katika Hoteli  hiyo  kilichoandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa .

Alisema  kuwa lengo la  mkoa wa  Iringa ni  kuzidi  kutangaza utalii  wa mikoa ya kusini kupitia mpango kabambe wa karibu  kusini  na kuwa  wao kama  wadau  wa sekta ya  Utalii wameendelea  kuboresha  huduma bora za Hoteli na ndio  sababu ya  kufungua  Iringa  Sunset Hoteli  ambayo ni hoteli  nzuri  inayovutia  wageni na wenyeji  kujiona kama  wapo  katika Hoteli  zilizopo  ndani ya  hifadhi  hapa  nchini .


Hivyo  alisema bado  Iringa Sunset Hoteli  inawaomba  wakuu  wa taasisi mbali mbali ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya  mkoa wanapohitaji  huduma  bora za chakula ,kumbi na sehemu  sahihi ya  kulala  wasisite  kufika mjini  Iringa na   kutembelea Iringa Sunset Hotel iliyopo  eneo la Gangilonga  jirani na  shule ya msingi Mapinduzi 


Wajumbe wa kamati   hiyo ya bunge ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji wakiwa  na mwenyeji  wao mbunge wa Mufindi Kaskazin Mahamudu Mgimwa  walieleza  kuvutiwa  na  huduma  nzuri  za Iringa Sunset Hoteli .


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania