CURRENT NEWS

Tuesday, September 26, 2017

WAKURUGENZI MKOANI SINGIDA WAAGIZWA KUNUA CHAKI ZINAZOZALISHWA MKOANI HUMO


 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akishiriki kazi ya uzalishaji chaki wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi wakati wa ziara ya kikazi

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimkabidhi boksi tano za chaki Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi mara baada ya kutembelea na kukagua kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi wakati wa ziara ya kikazi

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kazi ya uzalishaji chaki wakati wa ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi kutembelea Kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum na Uzalishaji chaki cha Dober Color Kilichopo katika Kata ya Itigi-Majengo Halmashauri ya Itigi

    Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akisalimiana na Meneja wa kiwanda cha Uzalishaji chaki cha Dober Color Ndg Mukhtar Mahamood mara baada ya kuwasili kiwandani hapo

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akikagua mizinga ya nyuki mara baada ya kutembele kiwanda Uzalishaji chaki, Mafuta ya Alizeti na Asali cha Fahari Kilichopo katika eneo la Tambukareli Halmashauri ya Mji wa Itigi wakati wa ziara ya kikazi, Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu


Ukaguzi wa kiwanda cha uzalishaji Chaki

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akikagua eneo la kutunzia Unga wa Gypusm katika kiwanda cha uzalishaji Gypsum cha Sanjaranda, Halmashauri ya Itigi

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akizungumza kwa njia ya simu na mmiliki wa kiwanda cha uzalishaji unga wa Gypsum cha Sanjaranda Bw Rashid Said Rashid akiwa Dar es salaam ambaye alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa mpaka kufikia Januari 2018 uzalishaji wa Gypsum utaanza katika eneo la Sanjaranda, Halmashauri ya Itigi ili kurahisisha huduma hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akiwa kwenye shamba la Mkulima Juma Patrick na kujionea mikorosho inavyoharibika kwa kukosa dawa ambapo alizungumza kwa njia ya simu na muwakilishi wa Bodi ya Korosho akiwa Dar es salaam ambaye alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa dawa za kuua wadudu kwenye Mikorosho zitawasili kati ya Jumanne  Septemba 26 na Jumatano 27, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akionyesha chaki bora zinazozalishwa Wilayani Manyoni Mkoani Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi Mhe Ally Minja mara baada ya kuwasili Kwa ajili ya kutembelea Kiwanda vya usagaji unga wa Gypsum na uzalishaji chaki.
Miongoni wafanyakazi wa kiwanda cha  Uzalishaji chaki cha Dober Color wakiendelea na kazi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi


1 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha Uzalishaji chaki cha Dober Color Halmashauri ya ItigiNa Mathias Canal, Singida

Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa Mkoani Singida wametakiwa kuanzia Septemba 25, 2017 kuanza kununua chaki zinazozalishwa katika viwanda mbalimbali vilivyopo katika Halmashauri ya Mji wa Itigi Mkoani humo.

Pia Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeagizwa kufuatilia Halmashauri zitakazoendelea na hatua za manunuzi ya chaki nje ya Mkoa wa Singida ili ziweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu haraka iwezekanavyo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi mara baada ya ziara ya kikazi ya kutembelea kiwanda cha uzalishaji Gypsum cha Sanjaranda, Kiwanda cha usagaji wa unga wa Gypsum/Uzalishaji chaki cha Dober Color na Kiwanda cha uzalishaji chaki cha Fahari.

Mhe Nchimbi alisema kuwa ni aibu kwa Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla kuagiza chaki nje ya nchi ilihali mkoani Singida zinazalishwa chaki zenye ubora, zisizo na vumbi la kuwasumbua walimu na wanafunzi kuliko za nje ya nchi tena kwa kutumia malighafi za ndani ya nchi.
 
Alisema Wakuu wa Wilaya wanapaswa kusimamia zoezi hilo ili kutumia bidhaa bora zinazozalishwa ndani ya Mkoa kwani zitaongeza ufanisi wa ajira kwa wananchi na kuwa na uwezo wa kutengeneza soko la ndani ya Wilaya na Mkoa kwa ujumla.

Alisema hakutakuwa na maana yoyote katika Mkoa kama viwanda vinazalisha chaki lakini watumiaji wa chaki hawanunui bidhaa hizo badala yake wananunua katika maeneo mengine.
 
Mhe Nchimbi aliwasihi viongozi mbalimbali katika Wilaya na Mikoa mingine nchini kununua chaki zinazozalishwa mkoani Singida huku akitoa unafuu kwa mikoa jirani na Mkoa wa Singida ambayo ni Dodoma, Manyara na Tabora kutumia gharama za manunuzi pekee huku serikali ikisimamia gharama zote za usafirishaji kuwafikia wanunuzi katika mikoa yao.

Sambamba na hayo pia Mhe Nchimbi aliziagiza Halmashauri zote mkoani humo kutangaza katika vyombo vya habari bidhaa zilizopo ili kuwarahisishia watanzania kufahamu uzalishaji unaofanywa na Mkoa wa Singida kwani kwa kufanya hivyo wafanyabiashara na wawekezaji watatambua fursa zilizopo na kununua bidhaa mbalimbali jambo ambalo litakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla.
 
Aliwapongeza wamiliki kwa kuanzisha viwanda hivyo katika Mkoa wa Singida kwani vimesaidia wananchi kupata ajira na kuweza kupata kipato kinachowasaidia kuweza kujikimu katika maisha yao sambamba na kuongeza chachu ya pato la Taifa kwa kulipa kodi.

Katika hatua nyingine amewaagiza wataalamu wa kilimo Mkoani Singida wakisimamiwa na wakuu wa Wilaya kufanya utafiti wa mbegu bora za alizeti na mazao mengine ili kuongeza uzalishaji wenye tija kwa wakulima.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Wilaya ya Manyoni alisema kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa yatafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo ili kuongeza ufanisi katika uwajibikaji na ukuzaji wa uchumi katika Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Mhe Mtaturu alisema kuwa pamoja na serikali kuelekeza mazao ya kipaumbele nchini ambayo ni Pamba, Korosho, Chai, Tumbaku na Kahawa lakini pia utasisitizwa uzalishaji wa zao la Alizeti ambalo limekuwa zao tija kwa wakulima na zao kubwa la biashara katika Mkoa wa Singida.
 
MWISHO.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania