CURRENT NEWS

Wednesday, September 20, 2017

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA DAKAWA WAPANIA KUFANYA VIZURI KWENYE MITIHANI YAO KIDATO CHA SITA MWAKANI.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo ya shule ya wasichana Dakawa kutoka kwa Makamu Mkuu wa shule hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu ya Shule ya sekondari ya wasichana Dakawa.

 Wanafunzi wa shule ya wasichana Dakawa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa akizungumza nao.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu ya Shule ya sekondari ya wasichana Dakawa.
............................................................................
WANAFUNZI wa kidato cha sita katika sekondari ya wasichana Dakawa iliyopo mkoani Morogoro wamepania kuwashangaza watanzania katika matokeo ya mwaka ujao ya kidato cha sita kwa kuifanya shule hiyo kwa miongoni kwa shule 20 bora kitaifa baada ya matokeo yao.

Wasichana hao wametoa  kauli hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Saidi Jafo alipofanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo ili kujionea mazingira halisi ya kufundishia na kujifunzia.

Shule hiyo kwa mwaka huu ilikuwa katika nafasi ya 69 kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita.

Kutokana na hali hiyo, Naibu Waziri huyo aliamua kufanya ziara hiyo kushtukiza ili aweze kubaini kama kuna changamoto kubwa  zinazo wakabili wanafunzi katika shule hiyo kwa kuwa ni shule ya wasichana pekee.

“Nimeona nije kujionea mwenyewe kama mambo mazito yana wakwaza ambayo yanaweza kumkwamisha mtoto wa kike asipate elimu inayo tarajiwa,”amesema Jafo 

Katika ziara hiyo, Jafo alifanya ukaguzi wa madarasa, mabweni, nyumba za walimu, jiko, vyoo, maktaba, na bwalo la Chakula.

Jafo aliwaambia walimu na wanafunzi kwamba serikali ipo katika mpango kabambe wa shule zote kongwe hapa nchini ili ziwe na mazingira mazuri ya utoaji wa elimu bora hapa nchini.

Aidha Naibu Waziri huyo ameonesha kufurahishwa na suala la utunzaji wa mazingira ya shule ambapo wanafunzi na maeneo yote ya shule ni safi na yanavutia.

 Naibu Waziri Jafo anaendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya barabara, afya, Elimu, Maji na kuzungumza na watumishi katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Songwe na Tabora.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania