CURRENT NEWS

Saturday, September 30, 2017

WANANCHI WA KISANGIRE,KIHARE, TITU,KOLESA NA VIKUMBURU WILAYANI KISARAWE WAPATA MKOMBOZI.


Wananchi wa Vijiji vya Titu, Kisangire, Kihare, Kolesa na vikumburu wilayani Kisarawe wanatarajia kupata ukombozi kupitia mpango kabambe wa ujenzi wa barabara ya Chole - Titu - Kihare hadi vikumburu utakaoanza muda wowote ndani ya mwaka huu. 

Barabara hiyo imekuwa na changamoto kubwa miaka yote kutokana na kukosekana kwa daraja katika mto unaotenganisha kijiji cha Titu na Kisangire pamoja na kuwepo kwa tifutifu kubwa kwa eneo lote la barabara kitendo kinachosababisha wananchi wa maeneo hayo kupata shida kubwa ya kusafiri.

Katika ajenda ya kusukuma maendeleo, Mbunge wa Jimbo hilo Selemani Jafo amehangaikia kuboresha barabara hiyo na kufanikiwa kupata ufumbuzi kwa wakazi wa maeneo hayo kwani barabara hiyo katika kupindi kifupi kijacho itajengewa daraja kubwa katika mto uliopo katika kijiji cha titu na kuirekebisha barabara yote kwa kuiwekea kifusi, makalavati na mifereji ili kuruhusu magari kupita kipindi chote cha mwaka.

Ujenzi huo unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.5 ambapo kazi hiyo inatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.


Katika kufanikisha hilo, Jafo amewataka wananchi wote kushikamana ili kuharakisha maendeleo wilayani kisarawe.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania