CURRENT NEWS

Friday, September 15, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AUDHURIA TAMASHA LA JAMAFEST NCHINI UGANDA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akipokelewa na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda Bi. Asha Abdalla Mwelekwa mara baada ya kufika katika ofisi hizo ili kuonana na  Kaimu Balozi ambaye ni Naibu Balozi  Elibariki Nderimo Maleko.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akaisaini kitabu cha wageni katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini Uganda mara baada ya kufika ofisini hapo, pembeni ni Kaimu Balozi ambaye ni Naibu Balozi nchini Uganda Balozi Elibariki Nderimo Maleko.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe alifanya mazungumzo na wajumbe wa kamati ndogo ya maandalizi ya Tanzania ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya Tamasha hilo.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akiangalia ngoma ya Utamaduni ya Kikundi cha Taifa cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati alipofika katika uwanja wa Uhuru Kololo kuangalia maonesho ya bidhaa za wasanii wa nchi mbalimbali Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 Mhe. Mwakyembe akiangalia bidhaa za wasanii mbalimbali wa Tanzania alipofika katika Uwanja wa Uhuru Kololo na aliwapongeza Watanzania hao kwa kuitikia wito wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli kwa kutekeleza sera ya Viwanda kwa kuonesha  uwezo walionao wa kutengeneza bidhaa mbalimbali zenye ubora kwa malighafi zinayopatikana nchini, aidha aliahidi kwamba wakati wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania litapokaa katika kikao chake cha mwezi wa Novemba 2017 wasanii ambao walishiriki maonesho ya bidhaa za sanaa Kampala wataalikwa Dodoma kwa ajili ya kufanya maonesho kama hayo ili kuonesha ubunifu wa Watanzania waliona juu ya kuzalisha bidhaa za sanaa.
 Mhe. Mwakyembe akipokea bidhaa ya sanaa ya ubunifu ya hot pot la kuwekea chakula wakati alipotembelea banda la Nchi ya Burundi.
  Mhe. Mwakyembe akiangnalia bidhaa za viatu vinavyozalishwa na wasanii wa Nchi ya Rwanda ambvyo vikanyagio vyake vimetengenezwa kwa matairi ya gari wakati alipotembelea banda la nchi hiyo.
 Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mwakyembe akitembelea banda na nchi ya Kenya na kuangalia bidhaa za nchi hiyo.
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mwakyembe akitetembelea banda na nchi ya Uganda na kuangalia bidhaa za nchi hiyo.

Ubalozi wa Tanzania Nchini Uganda pamoja na Watanzania wanaishi nchini humo wamepongezwa kwa hatua walizozichukuwa za kuungana na serikali yao ya kuhakikisha kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inafanikiwa kushiriki katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Uhuru  Kololo jijini Kampala nchini Uganda.

Waziri wa Habari utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alitoa pongezi jana katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Uganda alipofika kuonana na Kaimu Balozi ambaye pia Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Elibariki Nderimo Maleko na kupokea taarifa ya maandalizi yaliyofikiwa ya JAMAFEST kwa upande ushiriki wa Tanzania.

Mhe. Mwakyembe alisema Ubalozi wa Tanzania Nchini Uganda chini ya Naibu Balozi Maleko na Watanzania wanaoishi Uganda chini ya Mwenyekiti wa  Umoja wa Watanzania wanaoishi Uganda (UTU) Benjamini Lesile walionesha mfano bora wa kujali nchi yao kwa kuwashajihisha wafanyabiashara pamoja na Watanzania wanaoishi Uganda kutoa michango yao ambayo imeweza kufanikiwa  vizuri na kuwezesha Tanzania kushiriki JAMAFEST kwa ufanisi na kwa faida ya nchi yao.

Watanzania wanaoishi nchi Uganda kwa kushirikiana na Kampuni ya Hariss International LTD ya Mfanyabiashara Mtanzania waliweza kutoa michango yao ambayo ilisaidia pale nchi iliyoandaa maonesho ilishindwa kuwawezesha washiriki kama vile maji ya kunya na vinywaji baridi, mahema na usafiri ambapo zaidi ya katuni za maji na soda mia mbili pamoja na mahema vilitolewa na Watanzania hao, kwa hiyo aliwasisitiza Watanzania walio ahidi kuchangia kutoa michango yao kwa mujibu wa ahadi walizotoa. "Ninamshukuru Balozi Maleko, Kampuni ya Hariss International LTD , Mwenyekiti wa UTU Benjamin na Watanzania wanaoishi Nchini Uganda kwa uzalendo wao" alisisitiza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Bara Mhe. Mwakyembe aidha ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua iliyochukuwa ya kipekee ya kushiriki JAMAFEST kwa kuvishirikisha vikundi vya Utamaduni na Sanaa vya taifa ambavyo vilitia fora katika maonesho kwa kuonesha utamaduni wa Visiwani, kwa hiyo alisema kwamba katika matamasha yajayo vikundi vya Utamaduni na sanaa vya taifa vya Tanzania Bara vitashirikishwa. Zanzibar iliwakilishwa na kikundi cha Taarabu cha Taifa na kikundi cha sanaa cha ngoma cha Taifa.

Mwaka huu jumla ya Wasanii wa utamaduni na sanaa za ubunifu wa Tanzania wapatao 196 walishiriki Tamasha hilo kwa kuonesha bidhaa zao za ubunifu za Ngoma, Mavazi, nguo, wasarifu wa milango na makasha ya mbao, vyakula na Lugha ya Kiswahili.

Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki  (JAMAFEST) lengo lake ni kutafuta soko la bidhaa za ubunifu za utamaduni na sanaa sio tu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki bali hata sehemu nyingine za dunia kwani ni bidhaa zinazobeba zaidi soko katika sekta ya utalii ambazo zimekuwa zinalishwa kwa wingi katika nchi wanachama na kukosa soko. Tamasha hilo linafungwa leo Alhamis jioni.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania