CURRENT NEWS

Sunday, October 15, 2017

RIDHIWANI-KUNA UMUHIMU WA KUANDIKWA HISTORIA YA USHIRIKI WA WANABAGAMOYO KUHUSU MWL.NYERERE

Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete

Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo

Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amesema kuna umuhimu wa kuandikwa historia na ushiriki wa Wanabagamoyo katika makuzi na siasa ya hayati Mwl.Nyerere .

Amesema historia ya Tanganyika kupata uhuru huwezi kutenganisha Uhuru wa watu wa Bagamoyo na maisha ya baba wa Taifa kwani yapo aliyofanya akipitia Bagamoyo .

Alibainisha hayo ,wakati wa siku ya kumbukumbu ya kifo cha baba  wa Taifa aliyetutoka miaka 18 iliyopita ,ambapo chama cha mapinduzi (CCM)wilayani Bagamoyo kiliadhimisha huko Lugoba .

Ridhiwani ambae alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo ,alieleza Mwl .Nyerere aenziwe kwa kuigwa kimatendo .

Alisema kwamba,wakati akikumbukwa hayati Mwl.Nyerere ni vyema upendo,mshikamano na demokrasia ikadumishwa miongoni mwetu .

Mwl.Nyerere aliwahi kufunga kwa ajili ya kupigania uhuru wetu, na pia kuswali na baadhi ya mashehe .

"Aliwahi kulala ,kuzungumza na kusali kata ya Mandela pale Mission akitokea Miono aliwahi kwenda Mandela Msalabani ambako alikutana na kijana mmoja ambae alizungumza nae ambapo kijana huyo ndie alikuwa dereva wake 1972-1980 " alisema Ridhiwani.

Nae mzee Mwalimu Akida ,ambae aliwahi kushuhudia mengi katika uongozi wa muasisi wa Taifa ,hayati Mwl.Julius Nyerere ,aliwataka viongozi ndani ya CCM kuacha visasi na kuwekeana chuki bali wafanyekazi kama timu moja ili kudumisha chama.

Aidha aliwasihi kujenga tabia ya kuwafuata wanachama kuanzia kwenye mashina badala ya wanachama kuwafuata wao maofisini ,;jambo litakalowasaidia kuzijua kero zinazowakabili na kuweza kuzitafutia ufumbuzi 

Mzee Akida alieleza ,uongozi ni dhamana na kioo cha jamii hivyo kila mmoja ajitambue na kuachana na visasi na chuki ambazo zitachangia kudidimiza maendeleo ya chama .


Hata hivyo ,mzee Akida alisema Mwl.Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa wa kupanga mambo ,alichukia uhasama,ubaguzi ,ukabila,majungu ,rushwa na alipenda kutenda haki na kusisitiza umoja .

,,:;Mwaka 1959 mie nilimaliza shule pale Mwambao,mwaka 1962 nilikuwa idara ya mapokezi MANTEP na pamoja na kufanya mazungumzo,alipokuja aliacha kitabu kinaitwa TUJISAHIHISHE";

" Katika kitabu hicho ukurasa wa kwanza kunaeleza umoja ambao ukidumishwa kutakuwa na mafanikio ,yawezekana kuna makosa tunayoyafanya na tofauti na watakavyoyafanya wengine ,ukimtilia mtu mashaka ,na anaekutilia mashaka ni jambo la kawaida"

"Hivyo msilipiane visasi kwenye uongozi ni mwikoo,pendaneni,mkifanyiana visasi mtayumbisha mema ambayo mmepanga kuyatekeleza kwa wananchi" alisisitiza mzee Akida .

Enzi za mwl.Nyerere walisoma bure,kula bure na kupata ajira kirahisi sanjali na vitu vingine muhimu bila kugharamia.

Mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani ,Subira Mgalu aliutaka uongozi wa CCM wilayani humo kufuatilia utekelezaji wa ilani kwenye halmashauri za Bagamoyo na Chalinze kwa maslahi ya wananchi .

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa CCM Bagamoyo ,alhaj Abdul Sharif alielezea katika uongozi wake hatopenda kuona mwanachama ama kiongozi mwenye chembechembe za chuki ,fitna na majungu .


Alikemea makundi na kuomba mshikamano baina yao pasipo kutengana.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania