CURRENT NEWS

Wednesday, October 11, 2017

JAFO:WATUMISHI TAMISEMI BADILISHENI KASI YA UTENDAJI KAZI

1.      Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa na Naibu Mawaziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kakunda (kulia) pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za OR TAMISEMI mjini Dodoma na kufanya kikao na Watumishi.

1.      Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo, kulia ni Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda

1.      Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Joseph kakunda(kushoto) akisaini kitabu mara baada ya kufika Ofisini  ‘Ofisi ya Rais –TAMISEMI’ mjini Dodoma

1.      Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege akisaini kitabu mara baada ya kufika Ofisini, ‘Ofisi ya Rais –TAMISEMI, mjini Dodoma

1.      Watumishi wa OR-TAMISEMI wakifuatilia kikao na Waziri pamoja na Naibu Mawaziri (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TAMISEMI –mjini Dodoma.
................................................................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo leo kwa mara ya kwanza amekutana na kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo wa mjini Dodoma tangu Rais Dk.John Magufuli ameteue kutumikia nafasi hiyo, huku akiwataka kubadili kasi ya utendaji wao ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wananchi.

Jafo ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na watumishi akiwa ameambatana na Manaibu Waziri wake Joseph Kakunda ambaye atakuwa Naibu Waziri anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili na Josephat Kandege yeye ni Naibu Waziri anayeshughulikia Afya, Miundombinu, Viwanda na Uwekezaji kwenye mamlaka za serikali za Mitaa.

Amesema ni vyema watumishi hao wakabadili kasi ya utendaji kazi wao kwa kuwa Wizara hiyo ndio tegemeo kubwa la watanzania na ni Injini ya mabadiliko katika Nchi.


“Nilipokuwa Naibu Waziri nilipata ushirikiano mkubwa sana kutoka kwenu.Mimi style yangu ni kukimbizana kufanya kazi namshukuru sana Mhe.Rais kwa kunitengenezea timu nzuri ya kufanya kazi Tamisemi na tutahakikisha mambo yote yanatekelezeka,”amesema

Jafo amesema hatapendezwa na yeyote ambaye atafanya kazi kwa ulegevu, mazoea na kutozingatia muda na kuwataka kuhakikisha wanatimiza malengo yaliyowekwa.

“Tusiwe busy for nothing nataka tuwe busy for something. Nataka tufanye kazi kila mtu kwenye eneo lake aache historia sitaki tufanye kazi kwa mazoea na sitaki kuongoza ofisi isiyo na upendo tushirikiane vizuri,”amesema


Kadhalika, Waziri Jafo amewataka watendaji wa wizara hiyo kuangalia uwezekano wa kufanya mchujo wa wanafunzi ambao wamekuwa wakichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule za vipaji maalum nchini kila mwezi wa sita na 12 ili kuweza kuwapata wanafunzi wenye uwezo kiakili wanaopaswa kuwa kwenye shule hizo na kuweka alama maalum.


“Hivi kuna umuhimu gani wa kuwa na special schools kama hazifanyi vizuri?Tuna  shule 22 za special schools mimi nilidhani hizi ndio ziwe zinaleta ushindani lakini hazifanyi vizuri hasa kwenye matokeo ya kidato cha nne,”amesema Jafo.


“Kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye eneo la elimu Kakunda(Naibu Waziri) hizi ndo ndoto unazopaswa kuziota kuanzia leo, nataka kuona mwaka 2019 kwenye 20 bora ziwe ni shule za serikali lakini sio ziongoze shule binafsi kuanzia 1-20 haiwezekani,”amesema Jafo

Amewataka Wakurugenzi wote mnaosimamia elimu kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuwataka wakeshe wakiomba sasa ni kazi na kwamba haipendezi kuikuta shule kongwe kama Azania kuwa kwenye shule 10 zilizofanya vibaya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Kakunda amesema anachokihitaji ni ushirikiano wa kutosha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa Wizara hiyo ni muhimu kwa nchi.

Amesema mambo matatu anayoyahitaji toka kwa watumishi kuwa ni “clarity” kuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa Majukumu, Sera, Sheria, Program, Miongozo na kanuni mbalimbali na kwamba mtumishi atakayefanya makosa akiwa na uelewa huo atakuwa amefanya kosa kwa makusudi.


Naye, Naibu Waziri Kandege amewataka watumishi kuipenda kazi na kuhakikisha bajeti ya asilimia 20.7 inayotengwa na Serikali kwenye Wizara hiyo inakuwa na tija kwa wananchi kwa kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania