CURRENT NEWS

Thursday, October 5, 2017

MAVUNDE ATIA FORA MKUTANO MKUU CCM WILAYA

 Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika mkutano Mkuu wa uchaguzi CCM wilaya ya Dodoma mjini.

 Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi CCM wilaya waliohudhuria

 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma mjini aliyemaliza muda wake Paulo Luhamo akifungua mkutano Mkuu wa uchaguzi leo.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Christine Mndeme katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa wilaya.


 Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi CCM wilaya waliohudhuria
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akifurahi jambo katika mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa wilaya.
......................................................................................
MBUNGE wa Dodoma mjini Anthony Mavunde ameeleza mikakati iliyopo katika kukifanya Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Dodoma kiweze kujitegemea kuwa ni mpango wa ujenzi wa jengo la ghorofa nane ambalo litakuwa jibu katika kuinua uchumi.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa uchaguzi leo uliofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Hall wilayani Dodoma, Mavunde amesema pamoja na mpango huo ni vyema wana CCM wakawa na umoja.

Aidha amewataka kuendeleza mbegu inayoachwa na viongozi wanaomaliza muda wao kwa kufanya kazi kwa umoja,upendo na mshikamano ili hatimaye matunda mazuri ya mbegu iliyopandwa yaweze kuonekana.

“Ndugu zangu tukimaliza uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine na ukitaka kushinda lazima uwe na mpango wa kisiasa kwak ufanya mikutano ngazi ya kata na katika hili mimi kama mbunge kuanzia mwakani nitagawa vipasa sauti vitatu na spika za kusimama kwa kila kata ili kuwezesha kufanyika mikutano hiyo na baadae nitaangalia suala la usafiri,”amesema Mavunde.

Amewaomba wajumbe wa mkutano huo kuendelea kumshukuru na kumpongeza Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuivunja mamlaka ya ustawishaji makao makuu(CDA) ambayo ilikuwa ni kilio cha wakazi wa Dodoma na kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake wilaya ya Dodoma mjini Paulo Luhamo amewataka wajumbe kuzingatia maagizo ya chama kwa kutochagua mtu kwa ajili ya ukabila,dini wala rangi.

“WanaCCM wenzangu chagueni kiongozi atakayetoka ndani ya CCM na sio nje ya CCM,atakayefanyia kazi maamuzi ya CCM,na mimi pamoja na kwamba nitakuwa nje ya uongozi nitashirikiana na uongozi mpya usiku na mchana,mvua na jua ili kulinda heshima ya Dodoma kuwa makao makuu ya Chama na Serikali,”amesisitiza Luhamo.

Amewataka wana CCM kuachana na utaratibu waliokuwa nao wa kubadilisha mbunge kila baada ya miaka mitano na badala yake wamempa heshima Rais kwa kuendelea kumchagua Mavunde kama mbunge wao,kumlinda na kumuombea.

“Mbunge wetu anafanya kazi kubwa kwa ajili ya CCM,sisi tumekuwa na utaratibu wa kuleta mbunge kila baada ya miaka mitano tuache utaratibu huu,rais ametupa heshima ya kumchagua Mbunge wetu katika baraza la mawaziri heshima ambayo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1975,hivyo kama rais ametupa heshima hiyo nasi tuilinde,”amesema Luhamo.


Wagombea wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti ni pamoja na Adam Msendo, Stephen Mwanga na Robert Mwinje.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania