CURRENT NEWS

Monday, October 30, 2017

MBUNGE WA KIBITI ATOA VYAKULA/VIFAA VYA MTIHANI KWA SHULE ZA SEK JIMBONI HUMO

 Mbunge wa Kibiti ,Ally Ungando ,akitoa vifaa vya mtihani na vyakula kwa shule mbalimbali za sekondari jimboni humo kwa ajili ya wanafunzi watakaofanya mtihani wa kidato cha nne ,mwaka huu .(picha na Mwamvua Mwinyi)
 Mbunge wa Kibiti ,Ally Ungando ,akiwa na baadhi ya wanafunzi wa moja ya shule ya sekondari jimboni humo,baada ya kutoa vifaa mbalimbali vya mtihani na vyakula kwa ajili ya wanafunzi watakaofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.(picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti

Mbunge wa jimbo la kibiti ,mkoani Pwani,Ally Seif Ungando ametoa vifaa vya mtihani,mboga na vyakula kwa shule zote 12 za sekondari zilizopo jimboni humo ,vyote vikiwa vimegharimu sh.mil.nne.

Mbunge huyo ametoa vifaa na vyakula hivyo ,kwa ajili ya wanafunzi wanatakaoanza mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne mwaka huu .

Ungando alifikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake ya kutoa chakula kwa shule zote za sekondari za jimbo la Kibiti.

Alieleza kwamba, huo ni muendelezo kwani mwaka jana amefanya hivyo pia kwa shule zote .

Ungando alisema ni aliahidi kuchangia sekta ya elimu ,wakati anaomba kura wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa 2015 .

Pamoja na hayo atawazawadia vijana wote watakaopata alama A' ktk somo la sayansi kwenye mtihani huo.

Ungando alisema kuwa ,anaendelea kutatua na kusimamia kero mbalimbali zinazokabili sekta ya elimu ,afya ,miundombinu na masuala ya kijamii ikiwemo kuwezesha makundi maalum.

"Sitachoka na nitaendelea kusaidia na kutimiza ahadi nilizozitoa kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo hili " alisema.

Baadhi ya walimu na wanafunzi katika shule hizo ,walimshukuru mbunge Ungando kwa jitihada zake za kimaendeleo anazozichukua .

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania