CURRENT NEWS

Saturday, October 21, 2017

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA UMEME KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (wapili kulia), akifurahia jambo na wahandisi na mafundi wa TANESCO alipotembela  mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2017.
 Naibu Waziri, Mgalu, (katikati), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANSECO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), na Naibu Mkurugenzi Mtendjai wa TANESCO, (anayeshughulikia usafirishaji umeme), Mhandisi, Kahitwa Bishaija, (kushoto), wakiwasili kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kigamboni jijini Dar es Salaam Oktoba 20, 2017.
 Wahandisi wa TNESCO wakimalizia kazi ya kufunga mitambo kwenye kituo cha Kigamboni.

NA  K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, ameendelea na ziara yake ya kujifunza kwa kukagua miradi mingine miwili mmoja wa ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme Kimbiji na kingine cha kupoza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2017.
Alhamisi Oktoba 19, 2017, Mhe. Mgalu alifanya ziara kama hiyo kwa kutembelea vituo viwili vya kupoza umeme vya Mbagala na Kurasini wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiwa KIgamboni, Mheshimiwa Naibu waziri ambaye alifuatana na Katibu Tawala wa Wilaya mpya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na viongozi wengine wa juu wa Shirika hilo, alianza kwa kukagua kituo cha Kigamboni ambapo aliwakuta mafundi wa TANESCO wakimalizia kufunga mitambo kwenye kituo hicho.
Aidha Naibu waziri alimalizia ziara yake kwa kutembelea eneo la ujenzi wa kituo kipya cha Kimbiji ambapo kazi ya kusafisha eneo la ujenzi nayo imekamilika na kinachosubiriwa ni kuwasili kwa vifaa ili ujenzi uanze.
Mheshimiwa Mgalu alisema kutokana na ongezeko kubwa la watumiaji wa umeme, vituo hivyo vitasaidia sana kuboresha huduma ya upatikanaji umeme hususan katika kipindi hiki ambacho serikali ya awamu ya tano imejielekeza kujenga uchumi wa viwanda na hitajio kubwa katika utekelezaji wa mpango huo ni upatikanaji wa umeme wa uhakika.
“Niwashukuru tu kwa ksuema, ziara yangu hii ni ya kwanza kwenye eneo hiki tangu niteuliwe na nimeona nije ili nijionee jitihada hizi za kuboresha hali ya umeme wilayani Kigamboni ambapo kuna uhitaji mkubwa wa umeme ,kutokana na ongezeko kubwa la watu.” Alisema.
Akieleza zaidi Mheshimiwa Mgalu alihimiza Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ambalo kwa niaba ya serikali ndilo linatekeleza mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi ili hatimaye wananchi wapate huduma ya umeme katika hali bora zaidi.
Aidha Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, Aliishukuru serikali kwa kuleta mradi huo katika wilaya hiyo na kusema serikali wilayani Kigamboni itatoa kila aina ya msada ili kuhakikisha mradi huo mkubwa unakamilika.
“Hii ni wilaya mpya ni jambo la kushukuru kuwa katika kipindi kifupi wilaya inaletewa mradi mpya wa kuboresha umeme kwa kweli wananchi wana matarajio makubwa na mradi huu na sisi tumefarijika sana.” Alisema Katibu Tawala wa wilaya ya Kigamboni.


 Naibu waziri akipatiwa maelezo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi Kahitwa Bishaija, (wapili kushoto). Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Naibu waziri akipatiwa maelezo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi Kahitwa Bishaija, (wapili kushoto). Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (kushoto), akifurahia jambo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, wakati wakitoka ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo kuanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa vituo vya umeme vya Kigamboni na Kimbiji.
 Meneja Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (kulia), akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa Nihstai, Mhe. Subira Mgalu, (wakwanza kushoto) kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Kimbiji, wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, Oktoba 20, 2017.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula, (kulia), akimuonyesha mchoro wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kigamboni, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (katikati), na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, wakati Mhe. Mgalu alipotembekea kituo hicho leo.
 Mhe. Mgalu akizungumza jambo.
Picha ya pamoja mwishoni mwa ziara.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania