CURRENT NEWS

Tuesday, October 10, 2017

RAILA ODINGA AJIONDOA KWENYE UCHAGUZI MKUU KENYA
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ametangaza kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao unapangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
Bwana Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu
Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.
Bw. Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia ili nzuri.
Awali tume ya uchaguzi ilikuwa imemtangaza rais wa sasa Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.
Ilisema kuwa Bw. Kenyatta alishinda uchaguzi huo kwa kura milioni 1.4.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania