CURRENT NEWS

Monday, October 9, 2017

SERIKALI YAAGIZA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA ZILIZOPELEKWA KWENYE VITUO VYA AFYA NCHINI.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Maimuna Tarishi akifungua kikao cha kazi cha watendaji wa mikoa na Mamlaka za serikali za mitaa cha uboreshaji wa huduma za afya nchini.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tamisemi(Afya), Dk.Zainab Chaula akizungumza katika kikao cha kazi cha watendaji wa mikoa na Mamlaka za serikali za mitaa kilichofanyika mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza katika kikao cha kazi cha watendaji wa mikoa na Mamlaka za serikali za mitaa kilichofanyika mjini Dodoma.

Baadhi ya watendaji wa mikoa na Mamlaka za serikali za mitaa wakiwa katika kikao cha kazi. 

Viongozi mbalimbali wakiwa katika kikao cha kazi cha watendaji wa mikoa na Mamlaka za serikali za mitaa.
..................................................................
SERIKALI imezitaka mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha zinasimamia ipasavyo ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya 172 nchini ili kuweza kukamilika kama ambavyo imekusudiwa.

Hivi karibuni serikali ilitoa fedha kiasi cha Sh.Milioni 500 kwa kila kituo cha Afya.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Maimuna Tarishi alipokuwa akifungua kikao cha kazi cha watendaji wa mikoa na Mamlaka katika uboreshaji wa huduma za afya.

Amesema kuwa serikali haitamfumbia macho kiongozi au mtumishi yeyote ambaye atatumia vibaya fedha zilizotolewa kwa ajili hiyo.

Amewataka kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa vituo hivyo unakamilika kwa wakati na kwa kiwango kilichokusudiwa.

Tarishi amesema hatarajii kuona kuna mkurugenzi yeyote anakwenda kinyume na ramani za ujenzi zilizotolewa na serikali kwa madai kuwa fedha hizo hazitoshi.

Amefafanua kuwa serikali ipo katika mkakati wa ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma na kupunguza vifo vya mam na mtoto ambavyo hadi sasa vimefika vifo 556 kwa vizazi hai 100,000.

Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Mhandisi Mussa Iyombe, amesema kuwa sekta ya afya bado ina changamoto nyingi ikiwemo majengo.


Amesema serikali imedhamiria kutatua changamoto hizo ambapo ujenzi pamoja na ukarabati huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 30 mwaka huu na tayari fedha zimepelekwa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania