Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki Dua
maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya
Dodoma.
Washiriki wa Dua maalum katika Madrasa ya Darul
Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza
katika Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa
ya Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa kwenye
picha na viongozi wa dini
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisikiliza
mawaidha katika Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul
Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma
.........................................................................
Viongozi mbalimbali na waamini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya
Dodoma Mjini,wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde
kwa utendaji kazi na kuleta maendeleo katika Jimbo hilo.
Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa Dua maalum iliyofanyika
katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe.
Viongozi hao wamempongeza Mbunge Mavunde kwa kugawa vitabu vya
Misahafu 50,Juzuu 400 na Kanzu 300 katika misikiti mbalimbali hapa Dodoma Mjini
na kwa kusimamia mabadiliko makubwa katika sekta za Afya, Elimu,
Miundombinu,Michezo na Uwezeshaji wananchi.
Akitoa maelezo ya awali,Mwalimu wa Madrasa Ustadhi Omar Salum
Itara amemshukuru Mavunde kwa msaada mkubwa alioutoa katika Madrasa hiyo ikiwa
pamoja na kuwawekea umeme ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza mpaka
usiku.
Kwa upande wake, Mavunde akizungumza katika Dua hiyo, amewashukuru
Viongozi na waamini wa dini ya kiislamu kwa namna wanavyomuunga mkono katika
shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo na kuwaomba waendelee kumuombea kwa
Mwenyezi Mungu atimize majukumu yake vyema.
Mavunde ameipa Misikiti 16 Spika moja kila mmoja zenye thamani
ya Tsh 4,000,000 na pia ameahidi kukabidhi Laptop 2 zenye thamani ya Tsh
1,000,000 na milango miwili yenye thamani ya Tsh 500,000 kwa ajili ya madrasa ya
Darul Mustafa.
Post a Comment