CURRENT NEWS

Saturday, October 21, 2017

WAFANYABIASHARA KATIKA VITUO VYA MWENDOKASI WAONDOLEWE –WAZIRI JAFO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo (katikati) akikagua kituo cha Kivukoni wakati wa ziara yake katika vituo vya mabasi yaendayo haraka, kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka(DART) Leonard Lwakatare na  Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa miundombinu Eng. John Shauri .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo (katikati) akimskiliza mwananchi Bi.Salma Hoza(mbele) akitoa maoni yake kuhusu huduma inayotolewa na Wakala wa mabasi yanedayo haraka (DART)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo (katikati) akifuatilia mwenendo wa mabasi yaendayo kwa haraka(hayapo pichani) yanayofanya kazi katika vituo vya kushushia na kupakia abiria. 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo (kulia) akitoa maelekezo kwa wataalam wa wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) wakati wa ziara yake katika vituo vya Mabasi hayo kulia ni Mtendaji Mkuu wa DART Leonard Lwekatare.

.................................................
Nteghenjwa Hosseah – Tamisemi – Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo ameagiza wafanyabiashara wote wanaofanya biashara katika vituo vya mabasi yanaendayo haraka waondolewe na watafutiwe maeneo maalumu ya kufanyia kazi zao na halmashauri husika.

Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika vituo vya mabasi yaendayo haraka vya Morroco na Kivukoni na kukuta wafanyabiashara ndogondogo wakiendelea na shughuli ambazo kwa kiasi kikubwa zinaharibu na kuchafua miundombinu ya mabasi yaendayo haraka.

“Vituo hivi ni maalumu kwa ajili ya abiria kusafirishwa mpaka maeneo wanapokwenda na sio biashar na kwa sababu vituo hivi viko kwenye halmashauri ambazo nazisimamia Mimi naagiza wafanyabiashara hawa waondolewe na watafutiwe maeneo yatakayofaa kwa ajili ya biashara zao lakini sio ruksa kufanyia biashara hizo katika eneo hili maalumu kwa ajili ya mabsi yanedayo haraka” alisema Waziri Jaffo.

Katika ziara hiyo Waziri Jaffo aliagiza uongozi wa DART kufanya mazungumzo ya haraka na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani kuangalia namna bora ya kuongoza mabasi hayo kwenye maeneo ya makutano ya barabara hususan sehemu zenye Taa za kuongozea magari na ikiwezekana taa za barabarani zifanye kazi yake.

“Nimepokea malalamiko toka kwa wananchi ambao ndio watumiaji wa mabasi  kuwa husimama muda mrefu kwenye maeneo zilipo Taa za barabarani kwa sababu Askari anayaongoza yeye na sio taa hivyo husimama muda mrefu kusubiria Askari ayaruhusu na kupoteza maana ya kuwa mabasi yaendayo haraka” alisema Jaffo.

Aidha Waziri Jaffo aliutaka uongozi wa DART kuongeza Kadi za kusafirishia abiraia kwa sababu imekua ni hitaji kubwa sana na la muda mrefu la watumiaji wa usafiri huo: Hakikisheni mnakamilisha mchakato huo mapema ili wananchi wapate huduma hiyo wanayoihitaji.

Pia aliwasisitiza uongozi wa DART kuwaelekeza madereva wa mabasi yaendayo haraka kuhakikiasha wanachukua abiria katika vituo vyote na sio kuwaacha abiria katika baadhi ya vituo kwa sababu ya wingi wa abiria hayo na yale Mabasi ya Express kutoka Kivukoni –kimara na Gerezani-Kimara kuchukua abiria wa Kimara tu na si wale wa kushuka kwenye vituo vya karibu.


TAMISEMI YA WANANCHI.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania