CURRENT NEWS

Saturday, October 28, 2017

WAZAZI NA WALEZI WASIENDEKEZE KUCHANGIA SHEREHE ZAIDI KULIKO ELIMU-NSEKELA


Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo

WAZAZI wilaya ya Bagamoyo ,mkoa wa Pwani wametakiwa kuamka kwa kuona umuhimu wa kuchangia elimu pasipo kuendekeza kuchangia sherehe mbalimbali, ili kuwajengea msingi bora watoto wao katika sekta hiyo.

Meneja wa benki ya CRDB wilayani humo ,Nitike Nsekela aliyasema hayo kwenye mahafali ya 6 ya kidato cha nne shule ya sekondari ya wasichana ya Mandera ,Chalinze wilayani humo .

Alisema umefika wakati kwa wazazi na walezi kugeukia elimu kama ilivyokuwa katika sherehe na kuacha kuona elimu ni jukumu la serikali pekee .

Aidha Nsekela alikerwa kuwepo kwa tabia za baadhi ya wazazi na walezi kuwakatishwa masomo watoto wao wakike hali ambayo ni kumnyanyasa na kumnyima haki mtoto huyo .

Alieleza ,mwanafunzi wa kike kumkatisha masomo kisha kumuozesha kabla muda wake ni kuyeyusha ndoto yake.

Nae mwalimu Rose Umila akisoma taarifa ya shule alisema wanaotarajia kufanya mtihani wa kuingia kidato cha tano mwishoni mwa mwezi huu ni 98.

Alielezea kwamba ,wanakabiliwa na changamoto ikiwezo ukosefu wa bwalo la chakula, maabara, maktaba, ukumbi wa mikutano sanjali na uchakavu wa majengo yanayohitaji ukarabati.

"Katika ufaulu tumejitahidi kupandisha ufaulu kutoka wanafunzi 12 wa mwaka 2015 kufikia 27 mwaka 2016,"

"Shule hii ina wanafunzi 390, walimu 33 kati ya hao wa sayansi 7, sanaa 25, na biashara mmoja, wafanyakazi wasio walimu 7 ambao ni vibarua kati yao walinzi watatu, wapishi watatu na mlinzi mmoja," alieleza mwalimu huyo.

Shule hiyo ilianzishwa mwaka 2009, huku ikiwa na malengo ya kuhakikisha watoto wa kike wanapatiwa fursa ya kielimu.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania