CURRENT NEWS

Tuesday, October 10, 2017

WAZIRI JAFO ATETA NA WATUMISHI WA TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watendaji wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kubadili utendaji wao wa kazi ili kupata matokeo bora katika kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya TAMISEMI mara baada ya kuapishwa amesema biashara ya kufanya kazi kwa mazoea haina nafasi na maemtaka kila mtumishi kubadilika na kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokea tarajiwa.

Waziri Jafo amesema “ili tuweze kufikia malengo yetu kwa hataka na ufanisi wa hali ya juu naahidi kutoa  ushirikiano kwa kutosha kwa Manaibu Waziri waliochaguliwa na kuapishwa pamojanami leo hii, viongozi wengine wote wa Wizara, manajiment pamoja na watumishi wote.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Naibu Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe. George Joseph kakunda amesema TAMISEMI ni injini ya Nchi na isipofanya vizuri hakuna Wizara nyingine itakayofanya vizuri kwa sababu unapozungumzia tamisemi unagusa wananchi na mengine yote yanayofanyika katika Wizara nyingine ni kwa ajili ya wananchi hawa wa TAMISEMI hivyo ni lazima tuweke mazingira bora na rafiki ili huduma hizo ziwafikie zikiwa na ubora wa hali ya juu.

“Wizara hii ni muhimu sana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa sababu watekelezaji wa miradi mbalimbali wako katika mamlaka ya serikali za Mitaa hivyo tukifanya kazi kwa bidii na uaminifu hakika mafaniko yatakuja kwa haraka na hilo sisi ndio tunalolihitaji katika Serikali ya awamu ya Tano” alisema Mhe. Kakunda.Katika mabadiliko yaliyofanywa juzi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli Wizara ya TAMISEMI itaongozwa na Manaibu Waziri wawili ambao ni Mhe. George Joseph kakunda na Mhe. Josephat Sinkamba Kandege huku Waziri wa Wizaa hii akiwa ni Mhe. Selemani Said Jafo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ndogo ya TAMISEMI – Dar es salaam baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda na kushoto kwake ni Naibu Waziri Mhe. Josephat Kandege
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (aliyesimama katikati) akizungumza na wafanyakazi wa TAMISEMI ofisi ndogo ya dar es salaama mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika Picha ya pamoja ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (pili kushoto aliyekaa, Mhe. George Joseph kakunda (kwanza kushoto aliyekaa) Naibu Waziri Mhe. Josephat kandege(Pili Kulia aliyekaa), Naibu katibu Mkuu –Elimu Tixon Nzunda pamoja na watumishi wa TAMISEMI ofisi ndogo ya  Dar es Salaam.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania