CURRENT NEWS

Thursday, October 5, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AFUNGUA JUKWAA LA WADAU WA BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA SHINYANGA


Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe leo Alhamis Oktoba 5,2017 amefungua Jukwaa la wadau wa Biashara na Uwekezaji mkoa wa Shinyanga.
Jukwaa hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Uchapishaji Magazeti ya serikali (TSN) kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Shinyanga limefanyika katika ukumbi wa CCM/NSSF ya zamani mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo wakiwemo wafanyabiashara na wawekezaji.
Akizungumza wakati wa kufungua jukwaa hilo Waziri Mwakyembe aliipongeza TSN kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Shinyanga huku akiwataka wakazi wa Shinyanga kutumia fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta kuinua uchumi wao.
“Jukwa hili limekutanisha wadau wa maendeleo na kuwapa fursa kujitambulisha upya kwa wadau na wateja wao ili wajue huduma wanazotoa ili kukuza uchumi wa mkoa na kuchangia pato la taifa,tunahitaji nchi ya viwanda lakini viwanda hivi vinahitaji malighafi,tujitokeze kuwekeza katika maeneo haya ili kuinua uchumi wa nchi”,alisema Mwakyembe.
Alisema ili kufanikisha malengo ya Tanzania ya viwanda jitihada mbalimbali zinahitajika kwa kuwajumuisha wadau wote muhimu.
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN),Dr. Jim Yonaz alisema lengo la kuandaa jukwaa la fursa ni kuwaonesha wananchi kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo ya mkoa wa Shinyanga kwani wanahitaji kuona mkoa wa Shinyanga uwe kioo cha maendeleo kutokana na fursa zilizopo.  Dr. Yonaz alisema wameandaa jukwaa hilo la fursa ili kuchochea kasi ya uwekezaji mkoani Shinyanga.
Naye Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack alisema mkoa huo umetenga jumla hekta 22,099.12 kwa ajili ya uwekezaji wa miundombinu ya biashara,kilimo na viwanda.
Telack alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza katika kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa lengo la kupata mavuno yatakayotosheleza mahitaji ya viwanda vya kuchakata malighafi vilivyopo mkoani humo.
Aidha alisema kutokana na uwepo wa madini ya dhahabu,mkoa wa Shinyanga una fursa kubwa ya ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya madini ya dhabhabu.
“Natoa rai kwa wafanyabiashara wote wa ndani na nje ya nchi kuja katika mkoa wetu na kukamata fursa kwa kujenga viwanda na kufanya shughuli zingine nyingi za kuinua uchumi”,aliongeza Telack.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA
 Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakijiandaa kumpokea Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasili katika eneo la mkutano wa Jukwaa la wadau wa Biashara na Uwekezaji mkoa wa Shinyanga
 Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akipokelewa na viongozi wa mkoa wa Shinyanga
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe afungua Jukwaa la wadau wa Biashara na Uwekezaji mkoa wa Shinyanga
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza katika jukwaa hilo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akielezea fursa mbalimbali zilizopo mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN),Dr. Jim Yonaz akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN),Dr. Jim Yonaz  akiteta jambo na Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN),Dr. Jim Yonaz akielezea malengo ya TSN juu ya jukwaa hilo la fursa
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN),Dr. Jim Yonaz akizungumza
Wafanyakazi wa TSN waliofanikisha Jukwaa la  wadau wa Biashara na Uwekezaji mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Dkt. Meshack Kulwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakiwa meza kuu
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Dkt. Meshack Kulwa akizungumza katika jukwaa hilo.
ENDELEA KUANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA MBALIMBALI HAPA CHINI
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania