CURRENT NEWS

Friday, November 3, 2017

CCM DODOMA YAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA CHIPOGORO KWA KISHINDO

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Alhaj Adam Kimbisa akimtambulisha Mgombea Udiwani Kata ya Chipogoro Hosea Fweda.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Alhaj Adam Kimbisa akimtambulisha Mgombea Udiwani Kata ya Chipogoro Hosea Fweda.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Alhaj Adam Kimbisa akimtambulisha Mgombea Udiwani Kata ya Chipogoro Hosea Fweda kwa wananchi.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Alhaj Adam Kimbisa na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde wakimtambulisha Mgombea Udiwani Kata ya Chipogoro Hosea Fweda kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni.

Mbunge wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akionyesha ujuzi wake wa kucheza ngoma za kigogo wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya Chipogoro.


 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Alhaj Adam Kimbisa akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani Kata ya Chipogoro .
Mbunge wa Jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akitoa somo kwa vijana na wananchi wa kata ya Chipogoro wakati uzinduzi wa kampeni za udiwani.
..........................................................................................................
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Dodoma kimezindua kampeni kwa kishindo kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Chipogoro huku kikiwataka wakazi wa kata hiyo kuendeleza heshima iliyopo ya Dodoma kuwa ngome ya CCM.

Katika uzinduzi huo kimepokea kadi za Chama Cha ACT Wazalendo mia nane ikiwemo kadi ya aliyekuwa katibu wa chama hicho mkoa wa Dodoma Weston Kaduma.

Akizindua kampeni hiyo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma alhaj Adam Kimbisa amesema siku zote Dodoma ni ya CCM hivyo watumie uchaguzi huo kumpa rais nguvu kwa kumchagua Hosea Fweda na kutoiyumbisha CCM.

“Juzi kuna chama kilikuja kuzindua kampeni zake hapa,kuna vijana walienda,nawapongeza vijana wale kwa kwenda kuwapa kampani lakini nina uhakika ndani ya mioyo yao wanasema wataipigia kura CCM, maana ndugu zangu mgeni akija kwako ukimuacha peke yake hatojisikia vizuri,”amesema  Kimbisa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde aliwataka wakazi wa Chipogoro kuimarisha umoja wao,kuepuka vurugu,kushauriana,kubishana kwa hoja na kumchagua diwani anayetokana na CCM ambaye ni Hosea Fweda.

“Ndugu zanguni mchagueni Hosea atetee shida zenu,awasilishe shida zenu kwa tajiri,sasa ukimchagua Jafari anapeleka wapi shida zenu kwa Mbowe?Mbowe apelekewe ana serikali?lakini ukimchagua Hosea awe diwani wa Kata hii kwa tiketi ya CCM atapiga mpira utapokelewa na mbunge,mbunge nae atapiga shuti kali mpaka golini ambapo ni kwa rais,”alisema Lusinde.

Kwa upande wake mgombea Fweda amewaomba wananchi wamchague ili ashirikiane nao katika kuwaletea maendeleo na kuahidi kuwa diwani wa Chipogoro katika kuwatumikia.

“Nichagueni mimi najua changamoto zilizopo katika kata hii ikiwemo ukosefu wa umeme,kituo cha afya na kwamba kwa kutumia viongozi na serikali ya CCM changamoto hizo tutazitatua,”alisema Fweda.


Mkoa wa Dodoma unafanya uchaguzi mdogo wa marudio katika kata moja ambayo ni ya Chipogoro.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania