CURRENT NEWS

Saturday, November 25, 2017

CCM YAHITIMISHA KAMPENI ZAKE KATA YA CHIPOGORO KWA KISHINDO

       

 wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Alhaj Adam Kimbisa katika mkutano wa kufunga kampeni Za Uchaguzi mdogo wa kata ya Chipogoro

Mwenyekiti wa CCM Dodoma Alhaj Adam Kimbisa akizungumza na wananchi wa kata ya Chipogoro.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika mkutano wa kampeni za udiwani kata ya Chipogoro.


Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika mkutano wa kampeni za udiwani kata ya Chipogoro. 
Mbunge wa Vitimaalum Agness Marwa akimnadi Mgombea udiwani Kata ya Chipogoro Hosea 

Wananchi wakisikiliza sera za CCM kwenye mkutano wa kampeni
 
Wananchi wakisikiliza sera za CCM kwenye mkutano wa kampeni
 
Mbunge wa Kibakwe George Simbachawene akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Chipogoro

Wananchi wakisikiliza sera za CCM kwenye mkutano wa kampeni
 
Mbunge wa Kibakwe George Simbachawene akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni kata ya Chipogoro

                ..............................................................................................................................

Chama cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Dodoma kimehitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo katika kata ya Chipogoro huku kikiwaasa wanachama wake kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kurudi nyumbani kungojea matokeo.

Aidha kimewaomba wanachama hao kumchagua mgombea anayetokana na chama hicho ili aharakishe maendeleo.

Akizungumza katika mkutano huo,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma alhaj Adam Kimbisa amesema CCM ni chama kinachohubiri amani na utulivu na katika uchaguzi huo wanachama wake hawana sababu ya kukaa vituoni bali warudi nyumbani wasubiri matokeo yatangazwe na msimamizi wa uchaguzi.

"Sisi kazi yetu ni kupiga kura kazi ya kuhesabu na kutangaza matokeo ni ya wengine,hivyo mkimaliza kupiga kura rudini nyumbani mkaendelee na shughuli zenu kama kawaida,"amesisitiza Kimbisa.

Alisema CCM imejijengea misingi imara iliyoasisiwa na waasisi wake ambayo inaendelezwa na viongozi wake na hivyo kuwaomba wana Chipogoro kutofanya makosa kwa kuchagua mgombea wa chama kingine bali wamchague Hosea Fweda anayetokana na CCM.

America hofu kuwa amani itakuwepo na wasikubali kutishwa na mtu yoyote.

Kwa upande wake,Mbunge wa Kibakwe George  Simbachawene na Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde alisema wasiogope waende kupiga kura wakamilishe haki yao ya msingi na ya  kikatiba ya kuchagua.

Naye, mgombea wa CCM katika nafasi hiyo ya udiwani Fweda amesema ameomba nafasi hiyo kwa ajili ya kuwatumikia na sio kwa maslahi yake binafsi na kuwaomba kutofanya makosa ya kuchagua mgombea mwingine
bali wamchague yeye ili akamilishe mafiga matatu na kuharakisha maendeleo.

"Ndugu zangu nawashukuru sana,mlikuwa pamoja nami toka octoba 27 tulipoanza kampeni zetu,na mmeandelea kuwa nami mpaka leo,nawaomba msiniache nichagueni mimi ili nikamilishe mafiga matatu,nawashukuru wagombea wenzangu wote niliokuwa nao katika mchakato huu,"amesema Fweda.

Kata hiyo inafanya uchaguzi baada ya diwani wake aliyekuwepo Raphael Temaluje  kufariki dunia.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania