CURRENT NEWS

Monday, November 6, 2017

DC WA HANDENI MH GODWIN GONDWE APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA ZAHANATI WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 14.7

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amepokea msaada wa vifaa vya ujenzi wa zahanati wenye thamani ya Shilingi Milioni 14.7 za Kitanzania kutoka Darworth Ltd, Mwekezaji wa kiwanda cha usindikaji matunda, kama shukurani baada ya kupewa ardhi yenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho Kitongoji cha Mkomba katika Kijiji cha Michungwani Wilayani Handeni..

Akizungumza wakati wa mapaokezi ya vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi ngazi ya Kata kuhakikisha wanasimamia na kutumia vifaa kwa kadri ilivyokusudiwa na kwamba asitokee mtu yeyote kupindisha matumizi au kusimamisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Ameongeza kuwa yote hayo yanafanywa kwaajili ya wananchi wa Handeni na kwamba maendeleo hayana itikadi, hivyo roho ya maendeleo iliyopo waishikilie ili wasonge mbele kwa pamoja kwakuzingatia kuwa wanatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Gondwe amesema kuwa Mh.Rais ameagiza kuwepo kwa maeneo yanayotengwa rasmi kwaajili ya viwanda , na sisi kama viongozi tumejumuika kwa pamoja kusimamia agizo la Mh.Rais, kwa Handeni ni wajibu wetu kuhakikisha tunaendelea kutenga maeneo kwaajili ya viwanda kama ambavyo kiwanda hiki kitakavyojengwa.

“Asitokee mtu akauondoa umoja huu, huu ni mwanzotu, viongozi tunakazi ya kuhakikisha vifaa hivi vilivyoletwa vinafanye kazi yake na wananchi waone matunda ya rasilimali yao” amesema Gondwe

Kadhalka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe ameahidi kusimamia na kuhakikisha vifaa vyote vinatumika ipasavyo na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji ili kufikia malengo ya ukamilishaji wa kiwanda cha kusindika matunda.

Kwa upande wake mwekezaji John Kessy kutoka kamupni ya Darworth Ltd amesema kuwa ujenzi wa kiwanda utakuwa si wa manufaa kwa wananchi wa michungwani tu, bali na hata kwao wawekezaji na ndiomaana wameona vyema kuchangia ujenzi wa zahanati sababu hata wafanyakazi watakaokuwa wanafanya kazi kwenye kiwanda watanufaika na huduma za afya zitakazotolewa hapo.

Aliongeza kuwa watafurahishwa kama vifaa hivyo vitasaidia kufikia lengo lililokusudiwa kwakuwa huo ni mwanzo na kwamba watendelea kufanya kazi bega kwa bega kwa kushirikiana na Serikali ili kufikia uchumi wa Tanzania ya Viwanda.

Mkuu wa Wilaya amepokea vifaa ambavyo ni Mabati (ya geji 28) 200, nondo Tani3,mifuko 200 ya saruji na mabomba lora 3 ambayo yatatumika kusambaza maji kutoka kwenye zahanati hadi kiwandani na kufanya jumla ya Mil.14.7, hatua ya ujenzi kwa sasa ipo kwenye michoro ambapo kiwanda kinatarajiwa kujengwa kuanzia Januari 2018 na kukamilika Desemba 2018. Mapokezi hayo yalijumuisha viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Wilaya hadi ya Kata.


Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia,Habari na Mawasiliano.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
4/11/2017 

 Mkuu wa Wilaya ya Handeni MH. Godwin Gondwe  (mwenye koti jeusi akipokea nondo kutoka kwa mwekezaji John Kessy kwa ishara ya kupeana mikono na viongozi wengine wakishuhudia
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni  kulia name Mwekezaji upande wa Kushoto akipokea mfuko wa saruji kuwakilisha mifuko mingine  ,pembeni ni viongozi mbalimbali wa Halmashauri
 Mapokezi ya mabomba kwa ajili ya kusambazia maji,  Mkuu wa Wilaya ya Handeni  mwenye koti jeusi akipokea kutoka kwa mwekezaji John Kessy, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza na uongozi wa Kata kwenye ofisi ya Kijiji cha Michungwani.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akizungumza kabla ya mapokezi ya vifaa na kumkaribisha mwekezaji Kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
 Mwekezaji John Kessy kutoka kampuni ya Darworth Ltd  akishukuru uongozi wa Wilaya kwa ushirikiano wanaoutoa katika kufanikisha Ujenzi wa kiwanda cha juice za matunda.
 Viongozi wakipokea nondo kwa pamoja
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania