CURRENT NEWS

Wednesday, November 22, 2017

HABARI KATIKA PICHA: MUENDELEZO WA ZIARA YA KUJITAMBULISHA YA RC MAHENGE KWENYE WILAYA ZA MKOA WA DODOMA

Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samwel Malecela (mwenye kofia ya njano) akimuonesha Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge mizabibu iliyopandwa kwenye shamba la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo


 Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakipata maelezo juu ya mashine ya kusukumia maji kwa ajili ya umwagiliaji wa matone kwenye shamba la zabibu la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo.
 Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua bwawa la kutunzia maji kwa ajili ya umwagiliaji wa matone kwenye shamba la zabibu la Chinangali II Wilayani Chamwino wakati wa Ziara ya Dkt. Mahenge Wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua nyaraka na kusikiliza kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Manzase  Wilayani Chamwino wakati wa ziara yake

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Manzase Wilayani Chamwino wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Mahenge (hayupo pichani) wakati alipofanya mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wananchi Kijiji hapo.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Ghorofa moja la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wakati wa ziara yake wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao akikagua chanzo cha chemichemi ya maji moto Mjini Kondoa, Chanzo hiko kwa sasa ndio kinategemewa kwa huduma ya maji Mjini Kondoa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania