CURRENT NEWS

Friday, November 17, 2017

JAFO AFUNGUA JENGO LA UTAWALA NA MAABARA MANISPAA YA TEMEKE

1.      Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(aliyesimama) akizungumza na watumishi pamoja na wananchi wa Manispaa ya Temeke(hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa Jengo la Utawala na Maabara iliyojengwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam.


 1.      Mratibu wa Miradi ya Benki ya Dunia inayosimamiwa na OR-TAMISEMI Erick Rodgers(aliyesimama kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jengo la Utawala na Maabara lilojengwa na Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam(kushoto kwake) ni Mratibu wa Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam katika Manispaa ya Temeke Edward Haule.
1.      Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kwanza kulia) akipokea Funguo kama ishara ya kukabidhiwa Jengo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva,Mratibu wa Miradi ya Benki ya Dunia inayotekelezwa na OR-TAMISEMI Erick Rodgers na Mratibu wa Miradi ya Benki ya Dunia  toka OR-TAMISEMI.

1.      Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akikata utepe kama ishara ya kufungua Jengo la Utawala - Manispaa ya Temeke, lililojengwa kupitia mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam(DMDP)

1.      Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Kushoto) akionyeshwa Ramani ya Jengo la Utawala –Manispaa ya Temeke alilolifungua mapema leo, na kulikabidhi wa Manispaa ya Temeke; Jengo hilo limejengwa na Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam. 

1.      Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Temeke,Wataalam na wananchi wakishuhudia Mhe.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.Selemani Jafo akifungua Jengo la Utawala lililojengwa kwa kupiia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam.

1.      Muonekano wa sehemu ya Jengo la Utawala –Manispaa ya Temeke lililojengwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam(DMDP).


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania