CURRENT NEWS

Saturday, November 18, 2017

JAFO ASITISHA MKATABA WA MKANDARASI WA BARABARA YA NAMELOK-SUNYA

1Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TARURA Bw.Victor Seif wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya kutoka Namelock hadi Sanya iliyopo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara.

1Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Sunya katikaWilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.


1Ujenzi unaoendelea wa Barabara ya Namelock hadi Sunya kwa kiwango cha Changarawe yenye urefu wa kilometa 88.1 zilizoko katika wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara.
...............................................................................................................................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Seleman Jafo amesitisha mkataba wa Mkandarasi Maginga Business Holding Co. L.t.d aliyekuwa akijenga barabara kutoka Namelok hadi Lopeltes kwa kushindwa kumaliza ujenzi huo kwa wakati wilayani Kiteto , Mkoani Manyara.

Waziri Jafo amefikia hatua hiyo baada ya kukagua na kutoridhishwa na kazi inayofanywa na Mkandarasi huyo.

Jafo amemuagiza Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura) kumpeleka mahakamani na kumfuta katika orodha ya wakandarasi , mkandarasi huyo kwa kutaka kuitapeli serikali.

Amesema kuwa mkandarasi huyo amekiuka makataba na kutaka kufanya utapeli kwa serikali kutokana kampuni yake kukosa wataalamu pamoja na vifaa vya kisasa kwajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo alitakiwa kujenga umbali wa kilomita 41.1 ndani ya miezi tisa lakini hadi sasa mkataba unaonyesha tayari amesha fanya kazi kwa miezi mitano na imebakia minne huku kazi ikiwa imefanyika kwa asilimia 7.

Amebainisha mkandarasi huyo katika kipindi cha miezi yake mitano alichoweza kufanya ni kusafisha eneo la kilomita 17 pekee na kushindwa kuifikia asilimia 50 ya mkataba wake.

Aidha,Waziri Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia miradi ya maendeleo nchini ili thamani ya fedha inayotolewa na Serikali iendane na thamani ya miradi inayotekelezwa nchini.

Jafo amesema kazi kuu ya Wakuu wa Mikoa nchini ni kusimamia maagizo yanayotolewa na serikali hasa katika suala zima la kusimamia maendeleo katika maeneo yao ili fedha zinazotolewa ziendane na kazi zinazotekelezwa katika jamii.


Kwa upande wake, Mtendaji mkuu wa Tarura Victor Seff, amesema kuwa maagizo ya serikali wameyachukua na watayafanyia kazi ili kuhakikisha kuwa fedha za serikali hazipotei kwa wakandarasi wababaishaji kama hao.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania