CURRENT NEWS

Thursday, November 9, 2017

JAFO AZINDUA KAMPENI YA VIWANDA VYETU, MKOA WETU KWA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

   
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Seleman Jafo akizindua  kampeni  ya kitaifa  ya uanzishwaji wa viwanda vidogo  na vya kati  katika Mikoa  na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye kikao cha Maafisa wa maendeleo ya jamii wa mikoa na Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Mjini DodomaWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Seleman Jafo akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Dk. Binilith Mahenge  muongozo wa uanzishwaji wa viwanda vidogo na kati wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na kati  katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  katika Kikao cha Maafisa maendeleo ya jamii wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini , mjini Dodoma

  
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo  wakiwa katika picha ya pamoja na Wari wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Uratibu, na Bunge  Mhe. Jenister Mhagama , Naibu Waziri wizara ya Viwanda na Bishara Mhe. Stella Manyanya  baadada ya kukabidhiwa muongozo wa uanzishwaji wa viwanda vidogo na kati wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na kati  katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  katika Kikao cha Maafisa maendeleo ya jamii wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini , mjini Dodoma


Baadhi ya Wakuu wa Mkoa kutoaka Mkoa wa Iringa, Singida, Manyara ,na Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Seleman Jafo(Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na kati  katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  katika Kikao cha Maafisa maendeleo ya jamii wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini , mjini Dodoma

    ........................................................................................................................
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezindua kampeni ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati katika Mamlaka za serikali za Mitaa na kuwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wanatimiza azma ya serikali ya kuhamasisha na kuanzisha viwanda hivyo kwenye maeneo yao.

Jafo amezindua kampeni hiyo ya kitaifa leo katika ukumbi wa chuo cha  Mipango ya Maendeleo Vijijini Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Maafisa wa maendeleo ya jamii wa mikoa na Halmashauri, Wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na viongozi mbalimbali.

Waziri Jafo amesema kila Mkuu wa mkoa anawajibu wa kuhakikisha azma ya serikali ya uchumi wa viwanda inatekelezwa kwenye eneo lake na kwamba watapimw utendaji wao wa kazi kupitia ajenda ya viwanda.

Amewataka Wakuu wa Mikoa nchini kuwahamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kuainisha na kutenga maeneo rafiki ya uwekezaji ili wawekezaji wanapokuja waweze kuonyeshwa maeneo  kwa haraka ambapo itasaidia kukuza uchumi katika ngazi ya Serikali za Mitaa.

“Kila Mkuu wa Mkoa atapimwa kulingana na viwanda ambavyo vimezalishwa katika mkoa wake kulingana na agenda ya kukuza uchumi wa viwanda nchini lengo likiwa  kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa wananchi” Amesema Mhe. Jafo.

Amesema  katika mwaka wa fedha 2016/2017  Halmashauri zote nchini zilitenga shilingi bilioni 53 kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wakina mama, zilizotolewa  hadi juni, 2017 ni shilingi bilioni 15.5 na tayari asilimia kumi zilishatolewa kwa vijana na akina mama wajasiriamali nchini lengo likiwa ni kuwawezesha kiuchumi na kupunguza umaskini nchini.

Mhe. Jafo amesema wakuu wa Mikoa wote nchini wanatakiwa kuwaongoza wananchi katika kuanzisha viwanda vidogo na vya kati ili kuweza kukuza uchumi na kuongeza ajira nchini na kupunguza umaskini kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.Jenista Mhagama amesema uchumi wa nchi umeendelea kukua lakini tatizo la ajira bado lipo nchini, kwa kuwa ajira rasmi imekuwa ikitoa asilimia 13 ya ajira zote katika nchi yetu na asilimia nyingine zimejikita katika sekta  isiyo rasmi na sekta ya kilimo.

Amesema kuwa sekta isiyorasmi inajumuisha wananchi  wenye kipato cha kati  na chini wanaojishughulisha  na kilimo, uvuvi, misitu na shughuli ndogondogo katika jamii, hivyo ili kuweza kupambana na upungufu wa ajira nchini ni lazima kutekeleza dira ya maendeleo ya mwaka 2025 inayoenda kwenye uchumi wa viwanda kuwa nimsingi wa kuondokana na umaskini nchini.

Kadhalika, Naibu Waziri Viwanda,biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya amesema Wizara ya Viwanda na Bishara  na uwekezaji  itaandaa muongozo maalum kwa ajili  kusimamia  ujenzi wa maendeleo  ya viwanda nchini  kwa Mamlaka za Mikoa na Wilaya.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania