CURRENT NEWS

Saturday, November 4, 2017

MPANDA MILIMA MASHUHURI KWA KUTUMIA BAISKELI DUNIANI, AMEANZA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

 MPANDA milima Mashuhuri kwa kutumia Baiskeli Duniani,Juanito Oiarzabal raia wa Hispania na wenzake wawili wameanza safari ya siku tano ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia lango la Kilema ikiwa ni aina mpya ya utalii iliyoanza kushika kasi katika hifadhi hiyo.


Hatua hiyo inatokana na jitihada za shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kueendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,kwa kuanzisha aina mpya ya bidhaa za utalii ili kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa watalii.Miongoni mwa bidhaa hizo ni pamoja na zile zilizoanzishwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimajaro (KINAPA) ya kuzunguka mlima kwa kutumia Parachuti pamoja na kupanda Mlima kwa kutumia Baiskeli, utalii ambao umeanza kushika kasi.Juanito Oiarzabal ambaye tayari ameweka rekodi nyingi duniani na kuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu kijulikanacho kama World Guinness Book amepanda mlima Kilimanjaro na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia kwa kutumia Baiskeli .Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA ) Ibrahim Musa amesema Oiarzabal atakuwa Mhispania wa kwanza kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia baiskeli na kwamba aina hi ya utalii ni rafiki kwa mazingira ya hifadhi.Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa inayoratibu wa changamoto hii a kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli,Mario Martos amesema hatua hii ni mwanzo wa kufungua aina hii ya utali katika Hifadhi za Taifa za Arusha na Saadani.Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro limeweka utaratibu wa kufanya vipimo kwa wapandaji wa Mlima kwa wanao tumia Baiskeli pia kabla ya kuanza safari ya kuelekea kileleni.Juanito na wenzake wawili wameianza safari ya siku tano ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia baiskeli wakipita lango la Kilema ambapo wanatarajia kupita katika Kilele cha Mawenzi kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea kilele cha Uhuru
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania