Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kulia)
akilakiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Dodoma Balozi Mstaafu Job Lusinde
alipomtembelea nyumbani kwake Uzunguni Mjini Dodoma, Balozi Lusinde
amemuhakikishia Dkt. Mahenge ushirikiano kutoka kwa wazee.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Dodoma Balozi Mstaafu Job Lusinde alipomtembelea nyumbani kwake Uzunguni Mjini Dodoma, Balozi Lusinde amemuhakikishia Dkt. Mahenge ushirikiano kutoka kwa wazee.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) akibadilishana
mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge wakati Dkt. Mahenge
alipomtembelea Mhe. Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge kwenye mradi wake mpya wa ufugaji samaki wakati Dkt. Mahenge alipomtembelea Mhe. Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimtembeza Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge kwenye mradi wake mpya wa ufugaji samaki
wakati Dkt. Mahenge alipomtembelea Mhe. Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya
mji wa Dodoma.
...................................................................................................................................
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge
amemtembelea na kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa
Dodoma Balozi Mstaafu Job Lusinde na kuhakikishiwa ushirikiano kutoka kwa Wazee
wakati wote wa uongozi wake Mkoani Dodoma.
Dkt. Mahenge alimtembelea Mwenyekiti wa Baraza la Wazee
Balozi (Mstaafu) Lusinde kwa lengo la kujitambulisha kama Mkuu mpya wa Mkoa wa
Dodoma na kuahidi kuwa atakutana na Baraza zima la Wazee la Mkoa wa Dodoma hivi
karibuni.
Kwa upande wake Balozi (Mstaafu)Lusinde amebainisha kumfahamu
Mheshimiwa Dkt. Mahenge kwa muda mrefu akiwa kwenye nafasi mbalimbali za
uongozi na kumpongeza kwa jitihada zake za kuongoza na kutumikia wananchi
kwenye nafasi mbalimbali alizowahi kutumika hivyo kumuhakikishia ushirikiano kutoka
kwa baraza la wazee.
“Wakati
wote wa uongozi wako hapa Mkoani Dodoma, Baraza la Wazee litakuunga mkono na
kukupatia ushirikiano mkubwa ili uweze kutekeleza majukumu yako hususani ya
kusimamia shughuli za maendeleo kwenye Mkoa wa Dodoma” alisisitiza Balozi
Lusinde wakati wa mazungumzo yake na Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge.
Aidha, Dkt. Mahenge
alipata pia fursa ya kumtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda
nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kujionea shughuli za kilimo
na ufugaji wa kisasa wa mifugo, nyuki na samaki.
Post a Comment