CURRENT NEWS

Tuesday, November 28, 2017

SPIKA JOB NDUGAI AONGOZA MAWAZIRI, WABUNGE NA VIONGOZI MBALI MBALI KATIKA MAZISHI YA ALIEKUWA MBUNGE WA SONGEA MJINI MAREHEMU MHE. LEONIDAS GAMA

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza Mawaziri, Wabunge pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.Viongozi mbali mbali waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Wanafamilia waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Viongozi mbali mbali waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Wapambe wa Bunge wakibabe mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama kabla ya kuzikwa leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Mke wa marehemu, Ndg. Esther Gama akiweka shada ya maua katika kaburi la mume wake, aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama, tukio lililofanyika leo makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiweka shada ya maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama aliezikwa leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Christina Mndeme (kulia) baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege cha Ruvuma tayari kuelekea katika mazishi ya aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama yanayofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akisalimiana na Meya wa Manispaa ya Songea, Mhe. Abdul Mshaweji (kulia) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songea mapema leo, tayari kuelekea katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama yanayofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Christina MndemeSpika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimfariji Ndg. Esther Gama mke wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama wakati wa mazishi yaliyofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.


PICHA NA OFISI YA BUNGE
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania