CURRENT NEWS

Saturday, November 4, 2017

TAARIFA KWA UMMA : MKUTANO WA MWAKA WA WATAALAM WA SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII 2017
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Simu Na.255-26 2963341/2963342/2963346
Nukushi: 255-26-2963348Barua Pepe:
ps@communitydevelopment.go.tz
Tovuti:www.mcdgc.go.tz           

Chuo Kikuu cha Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii,
Jengo Namba 11,
S.L.P 573,
40478 DODOMA.

                                                     

TAARIFA KWA UMMA
MKUTANO WA MWAKA WA WATAALAM WA SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII 2017
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, inataarifu umma kuwa itaendesha Mkutano wa Kazi wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Ngazi ya Taifa mwaka 2017 utakaofanyika Chuo cha Mipango Dodoma kuanzia tarehe 6 - 9 Novemba, 2017.
Ufunguzi wa Mkutano huo utafanyika siku ya Jumatatu Tarehe 6 Novemba, 2107 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na utafungwa tarehe 9 Novemba, 2017 na Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Madhumuni ya Mkutano huo ni kujenga uelewa wa pamoja wa wataalam wa maendeleo ya jamii kuhusu uzingatiaji wa maendeleo jumuishi katika kufikia uchumi wa kati na viwanda.  Kauli mbiu ya Mkutano wa Kazi mwaka 2017 ni: “AMSHA Ari ya Ushiriki wa Wananchi Kufikia Uchumi wa Viwanda”. Kaulimbiu hii imetokana na Wizara kuwa na nia dhabitti ya kuinua ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo yao na kupiga vita ukatili wa kijinsia ambao ni kikwazo katika kuleta maendeleo jumuishi.
Miongoni mwa matokeo tarajiwa ya Mkutano ya Sekta ya Maendeleo ni kupata mrejesho wa utekelezaji wa Sera ya Maendelo ya Jamii Nchini katika kuasha ari ya wananchi kushiriki kazi za maendeleo yao ili kufikia uchumi wa viwanda katika ngazi ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha, Mrejesho wa utekelezaji wa Mpango wa Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa mwaka (2017/18- 2021/22) katika ngazi za Mikoa na Halmashauri zote utatolewa na kujadiliwa; sanjari na kuamsha ari ya kushughulikia changamoto za ukatili na kuamsha ari na mbinu madhubuti zitakazo shirikisha jamii kikamilifu katika utatuzi wa migogoro ya kijamii.
 Washiriki wa Mkutano huu ni watumishi wa Wizara, Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wa Sekretarieti za Mikoa (26) na Mamlaka za Serikali za Mitaa (184), wawakilishi kutoka TAMISEMI, UNICEF na wageni kutoka Taasisi na mashirika mbalimbali.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)
04/11/2017
                                                       


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania