CURRENT NEWS

Monday, November 6, 2017

VIGUTA YAWAPIGA TAFU VIJANA PIKIPIKI 15 KIBAHA-KANYALLU

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MUUNGANO wa vikundi vya vicoba Tanzania (VIGUTA) umekabidhi pikipiki 15 kwa baadhi ya wanachama wa chama cha madereva wa pikipiki Kibaha mkoani Pwani( CHAMAWAPIKI )zilizogharimu milioni 30. 

Aidha VIGUTA imevitaka vikundi vya akinamama  vya vicoba kuhifadhi fedha zao kwenye taasisi za kifedha badala ya kutumia mfumo usio rasmi wa kuweka kwenye vibubu.

Akikabidhi pikipiki kwa vijana ambao ni madereva pikipiki Mailmoja-Kibaha ,Meneja Wa Viguta mkoani Pwani ,Iddi Kanyallu aliwasihi wananchi wakimbilie fursa zilizopo kwenye muungano huo.

Alieleza vijana hao walikopeshwa kwa gharama nafuu vyombo hivyo vya moto na kukabidhiwa ili kujiinua kimaendeleo .

Alisema hatua hiyo inalenga kuwawezesha vijana kuendelea kujiajili kupitia wenyewe badala ya kutumika na wamiliki ambao uwabana kimaslahi.

Kanyallu alisema ,wamekuwa wakitoa mikopo ya pikipiki kwa wajasiriamali vijana kwa rejesho la wiki sh.46,500 mkopo kwa muda wa mwaka mmoja .

"Tumekuwa tukishuhudia vijana hawa wakipewa Pikipiki na maboss wao ambapo hupeleka hesabu sh.70,000 kwa wiki lakini sisi tunakopesha kwa kuleta 46,500 kwa wiki "

"Sisi pia tunashughulika na vikundi vya akinamama wanatumia mfumo usio rasmi wa kuhifadhi fedha kwenye vibubu badala ya bank" alisema Kanyallu.

Pamoja na hayo ,alielezea kuwa ,Vicoba group union Tanzania inashughulika na NMB ambayo vikundi vyote husajiliwa na kuviunganisha kwa kupatiwa akaunti na kisha vinanufaika kwa kupata mikopo ya pikipiki,nyumba na mashamba.

Kanyallu aliwaomba ,waliokabidhiwa kutunza pikipiki zao ili kujiinua kiuchumi .

Nae mwenyekiti wa CHAMAWAPIKI -Mailmoja Kibaha,Ayubu Kijazi alisema chama kiliamua kwenda ofisi za Viguta huko Miembesaba na kupewa taratibu za kupata mikopo ya pikipiki.

Alisema kwamba ,kuna mikopo ya mikataba ambayo hutakiwa kurejesha kila siku sh.10,000 ikiwa ni 70,000 kwa wiki na ukitakiwa kumaliza mkopo ndani ya miezi kumi .

Kijazi alifafanua ,ipo mikopo ya pikipiki unayotakiwa kutoa asilimia 30 kisha 650,000 uirejeshe kwa mwezi.

Mwenyekiti huyo wa CHAMAWAPIKI aliishukuru Viguta kwa kuwafungua macho kwa kuweza kupata pikipiki zao wenyewe kujitafutia kipato .

 Meneja wa Vicoba group union Tanzania (VIGUTA)Mkoani Pwani ambae pia operesheni Meneja Taifa ,Iddi Kanyallu akimkabidhi mwenyekiti wa CHAMAWAPIKI -Mailmoja Kibaha,Ayubu Kijazi pikipiki 15 kwa baadhi ya wanachama wa chama cha madereva wa pikipiki Kibaha ( CHAMAWAPIKI )zilizogharimu milioni 30. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
 
Meneja wa Vicoba group union Tanzania (VIGUTA)Mkoani Pwani ambae pia operesheni Meneja Taifa ,Iddi Kanyallu akizungumza wakati wa makabidhiano ya pikipiki 15 kwa baadhi ya wanachama wa chama cha madereva wa pikipiki Kibaha ( CHAMAWAPIKI )zilizogharimu milioni 30. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Mbali ya hayo ,Kijazi alisema zipo changamoto wanazokabiliana nazo madereva bodaboda ikiwemo kuibiwa pikipiki hasa nyakati za usiku suala ambalo wanapambana nalo kwa kushirikiana na jeshi la polisi .

Kwa upande wake ,makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Focus Bundala alisema kwa vijana kupatiwa mikopo mbalimbali itawawezesha kujituma na kuondokana na kushinda vijiweni .

Alisema pikipiki hizo wamekuwa wakikopeshwa kupitia watu wengine kwa kulipia sh.mil.3 wakati Viguta imekuwa mkombozi kwani gharama zao ni nafuu.

Focus alieleza, halmashauri ya Mji huo inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya asilimia tano kwa vijana na wanawake asilimia tano ili kusukuma mitaji yao
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania