CURRENT NEWS

Tuesday, November 7, 2017

VIJANA WAMPA HEKO RAIS DK. MAGUFULI KWA MAFANIKIO MAKUBWA YA UTENDAJI NDANI YA MIAKA MWILI YA URAIS


Ndg Polepole akitoa mada kwenye Kambi hiyo
NA MWANDISHI WETU
VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametoa tamko la kumpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa mafanikio makubwa ya kiutendaji katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka yake mwili ya Urais.

Tamko hilo limetolewa  katika kambi ya Vijana iliyokuwa ya siku tatu ilijumuisha vijana 500 kutoka Vyuo na Vyuo vya  Vikuu nchini na Vijana kutoka Matawi katika Kata zote mkoani Mwanza  ikiwa na lengo la kujenga vijana kuwa na uzalendo, maadili bora, uongozi na kuijua vyema itikadi ya Chama Cha Mapinduzi lengo likiwa kuwafanya pia watambue walikotoka walipo na wanakotaka kwenda.

Kambi hiyo ya Vijana iliandaliwa na kuratibiwa na Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu kupitia Seneti ya Vyuo katika mkoa huo.

Akitoa mada, mtoa mada mkuu kwenye kambi hiyo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole aliwataka  Vijana kuwa wazalendo katika taifa lao na kuwataka wasitumike katika kukiharibu chama bali wawe walinzi na wasimamizi wa kukitetea chama na kukosoa watendaji wabovu wanaoiangusha serikali.

Polepole alisema, alisema, vijana wakijengeka katika misingi bora na kuijua vema itikadi ya CCM ndiyo wataweza kuwa na uzalendo, maadili mazuri na kisha kuwa viongozi bora. 

Akisoma maazimio ya kambi hiyo, Katibu wa Vijana mkoa wa Mwanza Mariam Amir alisema, Vijana waliokuwa kwenye kambi hiyo wameazimia kwa pamoja kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa mafanikio makubwa ya kiutendaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka yake mwili ya urais na kuahindi kuendelea kumuunga mkono ili kuhakikisha anafanikisha zaidi kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM.

Alisema, wameazimia hivyo kwa sababu Rais Dk. Magufuli katika kipindi hiki cha miaka miwili ameweza kusimamia mambo muhimu ya kuendeleza nchi ikiwemo katika sekta ya elimu, ujenzi wa reli standard geuge, ununuzi wa ndege, ujenzi barabara, bomba la mafuta, makusanyo ya kodi, udhibiti wa upotevu rasimali za umma  na nidhamu ya watumishi wa umma.

Mariam alisema Vijana pia wameazimia kuitumikia CCM kwa moyo na nguvu zao zote na kuahidi kuwashughulikia wote wanaokwenda kinyume na maelekezo ya Chama na kutokubali kutumikia mtu zaidi ya kutumikia chama na kuahidi kupeleka ngazi za chini elimu na maarifa ya mafunzo waliyoyapata kutoka kambi hiyo kwa wanachama hasa vijana katika ngazi ya matawi na mashina ili kuendelea kuimarisha itikadi ya chama.

Alipokaribishwa kuzungumza  kwa nafasi yake ya Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu, iliyoandaa kambi hiyo, Daniel Zenda  aliwakumbusha vijana wajibu wa kila mwanachama katika kukisemea chama na serikali yake katika mafanikio yaliyotekelezwa kupitia ilani ya CCM

Zenda aliwataka pia vijana nchini kote kupambana kwa vitendo na wale wote wanaojaribu kubeza na kupotosha ukweli kuhusiana na jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Alisema umefika wakati sasa wezi na wanaotumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao sasa kujondoa weneyewe ndani ya Chama kwa kuwa CCM Mpya imeimarisha misingi yake chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli na sasa siyo kichaka cha kujifichia wezi.

"Bila shaka mmeshuhudia baadhi wakianza kuondoka wenyewe ndani ya CCM, sasa subirini watazidi kuondoka wezi wengi ndani ya CCM maana kwa sasa hawana namana ya kufanaya zaidi ya kukimbia", alisema Zenda.
Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Daniel Zenda akizungumza na Vijana katika kambi hiyo.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akitoa mada kwenye kambi hiyo
 Vijana katika Kambi hiyo wakinyoosha mikono kuunga mkono maelezo ya Polepole wakati akitoa mada 
 Viongozi meza kuu. Kushoto ni Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Daniel Zenda, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole
 Vijana wakikiliza mada
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza  na vijana kwenye kambi
Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Raymond Mangwala akizungumza kwenye kambi hiyo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania