CURRENT NEWS

Saturday, November 4, 2017

WAZIRI WA HABARI AMEFUNGUA MAFUNZO YA WATAALAM WA MICHEZOWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe  leo tarehe 4 Novemba, 2017 amekuwa mgeni rasmi  kwenye kufunga mafunzo ya Wataalam wa Michezo Wilayani Kyela, mkoani Mbeya. 

Katika shughuli hiyo, jumla ya wahitimu 128 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Baraza la Michezo la Taifa kwa kushirikiana na Chuo cha Michezo Malya. Akiwatukunu vyeti wahitimu hao, Waziri Mwakyembe amewataka kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia mafunzo waliyoyapata.
 "Kama tunavyofahamu michezo hutukinga na magonjwa pamoja na kuboresha afya zetu, lakini kwa sasa michezo ni ajira ya kuaminika na chanzo kikubwa cha mapato hivyo mkaisimamie vyema ili kupata matokeo chanya kwenye jamii yetu pamoja na kutengeneza wanamichezo watakaoliwakilisha taifa letu kimataifa", alisisitiza Mhe. Mwakyembe. Kwa upande wao, wahitimu wameshukuru kwa kuandaliwa mfunzo hayo na kuahidi kuwa walimu na mabalozi bora wa michezo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania