CURRENT NEWS

Tuesday, December 5, 2017

AWESO AKAGUA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI LONGIDO

1Naibu Waziri na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo wakitoka kukagua chanzo cha maji cha MtoSimba kilichopo wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro kitakachotumiwa na mradi wa Longido.

1 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), Mhandisi Ruth Koya (kushoto), Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo wakiangalia hatua ya ulazaji wa mabomba ya mradi wa Longido, mkoani Arusha.


 Naibu Waziri na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo katika sehemu ya mradi wa Longido, mkoani Arusha.
1     Ujenzi wa tenki la mradi wa Longido ukiendelea, mkoani Arusha.
.........................................................................................................
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, JumaaAweso ametembelea mradi wa maji wa Longido, katika Jiji la Arusha kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wake.

Naibu Waziri Aweso ameweza kujionea maendeleo ya mradi huo kwa kukagua ujenzi wa chanzo cha maji cha Mto Simba, kilichopo wilayani Siha, katika mkoa wa Kilimanjaro, ulazaji wa mabomba yenye umbali wa kilomita 65 mpaka Longido na ujenzi wa tenki la maji la lita 450,000.

‘‘Nimekuja Longido kuangalia hali ya utekelezaji wa mradi huu, lakini sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wake. Na mimi kama msimamizi wa miradi ya maji, hatuna budi kuchukua hatua sahihi ilimradi huu ukamilike kwa wakati’’, alisema Aweso.

‘‘Nitazungumza na Katibu Mkuu aweze kufika hapa, ili kutatua changamoto za mradi huu nakukamilika. Ni lazima mradi huu ukamilike na wananchi wa Longido waanze kupata maji nakumaliza adha wanayoipata sasa kama Serikali ilivyoahidi. Kuna haja ya wakandarasi wanaofanya kazi hii kuongeza kasi ili wamalize kazi waliyopewa.’’, alisisitiza Naibu Waziri.

Wakati huo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongollo amesema kuwa yeye pamoja na uongoziwa wilaya hiyo utahakikisha unasimamia ipasavyo ujenzi wa mradi huo naikibidi kuchukua hatua stahiki kwa mkandarasi atakayekwamisha mradi huo kukamilika kwa wakati.


Mradi wa maji wa Longido unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji nakusimamiwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji laArusha (AUWSA), ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na fedha za ndani za Serikali unaotarajiwa kugharimu kiasi cha Sh. bilioni 15.8 na kukamilika Mei, 2018.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania