CURRENT NEWS

Tuesday, December 5, 2017

CCM IRINGA WAPIGA KURA KUCHAGUA UONGOZI MPYA LEO

Mjumbe wa NEC Mh. Januari Makamba akizungumza na kutoa utaratibu wa wagombea na wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa unaofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa leo Chama cha mapinduzi kimekuwa na chaguzi za ngazi mbalimbali kuchagua viongozi watakaokwenda kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano tutawaletea taarifa zaidi kuhusu matokeo ya uchaguzi huo. 


Wagombea wa nafasi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika uchaguzi hu.
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo.
Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni mjumbe wa wa NEC na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza wakiimba wimbo kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa Uchaguzi.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Iringa na Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Bw. Richard Kasesela akicheza na mmoja wa wajumbe katika mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wakiimba nyimbo kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa uchaguzi mjini Iringa.
Mjumbe wa NEC na Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Iringa akicheza na mmoja wa wajumbe wenzake katika mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano huo wakicheza na kuimba.
Mmoja wa wagombea wa UNEC Bw. Salim Abri Asas akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa jimbo la Mufindi Mh. Mahmoud Mgimwa.
Wagombea nafasi ya Uenyekiti wa mkoa wa Iringa kutoka kushoto ni Albert Chalamila, Evance Balama na Daniel Kidava wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kujieleza kwa wajumbe.
Mgombea nafasi ya Uenyekiti wa mkoa wa Iringa Albert Chalamila akijieleza kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi huo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania